• Pasta huyo aliitwa kuwakemea mapepo waliokuwa wakimsumbua bwana mmoja kwenye boma lake na hakusita kufika kwa kazi hiyo
  • Baada ya kuchukua sadaka na kuanza kufanya maombi, nyoka wawili walitokea ghafla na kumshambulia pasta huyo hadi akatoroka mbio na kutokomea
  • Inadaiwa nyoka hao walitoweka kimuijiza baada ya nyimbo na kuwaacha wengi vinywa wazi wengine wakitoroka kwa uoga mwingi

Hali ya kutatanisha ilizuka Kasikeu, Makueni wakati Pasta aliyeitwa kuwakemea mapepo aliposhambuliwa na nyoka katika boma ya jirani ya muumini wake.

Pasta Achana Mbuga Baada ya Kuvamiwa na Nyoka Ghafla Akikemea Mapepo Katika Nyumba ya Muumini
Mchungaji kutoka Afrika Kusini Alph Lukaku aliyedai kumfufua mtu aliyekuwa ameaga dunia. Picha: Citizen TV
Source: UGC

Katika kisa hicho, mwenye boma hilo alimuendea jirani yake kumuomba usaidizi akilalamika kuhusu kusumbuliwa na mapepo.

Jamaa huyo alimuahidi kumletea mchungaji aliyesifika katika kuwakemea mapepo na kuwafukuzilia mbali na kumuondolea taabu ya mizimu hao.

Siku ya tukio hilo la kustaajabisha, mchungaji huyo alifika nyumbani humo tayari kuwa kuwakemea mapepo hao. Kabla kuanza maombi, alimuomba jamaa huyo kutoa sadaka ili kumpa Mungu haki yake na kufanikisha shughuli hiyo.

Jamaa alitoa KSh 5000 kisha pasta akaanza maombi huku akizunguka kila pande ya boma hilo. Alipofika nyuma ya nyumba hiyo, nyoka wawili walijitokeza ghafla na kuanza kumshambulia mchungaji huyo aliyetimka mbio kujinusuru huku akipiga nduru.

Pia soma

Wema Sepetu avunja ukimya kuhusu penyenye za IVF: “Niacheni, nimechoka”

Baada ya pasta huyo na waliokuwa wakishuhudia kukimbia, inadaiwa kuwa nyoka hao walitoweka kimuijiza na kuwaacha wengi vinywa wazi wasijue la kufanya.

Mwenye boma hilo alilazimika kujifungia ndani ya nyumba yake ishara ya kuogopa huku wenyeji wakidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa majoka hao.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *