
Mashariki mwa DRC, janga la Ebola sasa limesababisha vifo vya zaidi ya watu 300 miongoni mwa zaidi ya wagonjwa 1,200 wayothibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola. Katika mkoa wa Ituri, ulioathiriwa zaidi, miongoni mwa timu zinazofanya
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwandishi wetu maalum aliyerejea kutoka Bunia, Pascal Mulegwa
Katika mkoa wa Ituri, ulioathiriwa zaidi, miongoni mwa timu zinazofanya kazi ya kuvunja mnyororo wa maambukizi ni wafanyakazi wanaojitolea wa shirika la Msalaba Mwekundu wanaohusika na mazishi ya “heshima na salama” ya waathiriwa wa virusi hivyo, au wale wanaodhaniwa kuwa waathiriwa. Timu hizi mara nyingi hushambuliwa, wakati mwingine hujeruhiwa. Hata hivyo, katika mwezi mmoja, shirika la Msalaba Mwekundu linaripoti kuwa limefanya mazishi zaidi ya 300.
Ni saa 5 asubuhi huko Shari, nje kidogo ya jiji la Bunia, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Pembeni mwa nyumba, rundo la udongo limebadilishwa kuwa makaburi. Wachimbaji wa makaburi wanaanza shughuli yao, mhubiri anaanza kuimba nyimbo za dini.
Wafanyakazi wanne wa shirika la Msalaba Mwekundu, wakiwa wamelindwa kikamilifu na suti zao za kujikinga, wanamuingiza marehemu hadi kaburini.
“Hapo awali, tungemzika sisi wenyewe”
Wakati huu, ni ndugu wenyewe waliotoa taarifa kuhusu huduma za dharura, anaelezea Claude, mwanafamilia: “Sasa, tuna mashaka na kifo chochote… Tumeita shirika la Msalaba Mwekundu sisi wenyewe. Hapo awali, tungemzika sisi wenyewe.”
Kabla ya kila uingiliaji kati, timu ya upelelezi hutumwa kwenye eneo la tukio. Tahadhari ambayo imekuwa muhimu, kulingana na Alex Lock, afisa wa shirika la Msalaba Mwekundu. “Mahali tunapofanyia mazishi leo panaweza kuwa mahali pale pale tunapokabiliwa na jamii siku inayofuata. Ndiyo maana lazima tutumie timu ya upelelezi wa awali kwa utaratibu kabla ya kupeleka timu kufanya mazishi ya heshima na salama. Tathmini pia inajumuisha majadiliano na wanajamii na familia.” “Na mara tu ripoti itakapokamilika, ikiwa ni nzuri, tunatuma timu,” anaelezea.
Hata hivyo, wafanyakazi hawa wanajitolea wanatoka katika jamii wanazohudumia. “Baadhi ni walimu, wengine ni wafanyabiashara, watu waliofunzwa katika sekta ya afya, lakini si hao tu,” Alex Lock anasema.
Uhusiano huu wa karibu hurahisisha mazungumzo lakini unaendelea kukabiliwa na uvumi.
“Wanafikiri tunapata pesa nyingi baada ya kuzika mwili”
Kati ya kazi mbili, David, kiongozi wa timu, bado anajaribu kuwashawishi watau ambao bado wana mshaka karibu na makaburi. “Wanafikiri tunapata pesa nyingi baada ya kuzika mwili, wanasema dola 2,000,” anaeleza.
Ushahidi wa mvutano bado unaonekana: gari la kubeba maiti la shirika la Msalaba Mwekundu sasa linaendeshwa huku madirisha mawili yakiwa hayana vio, baada ya kuvunjika wakati wa tukio la wtu kurusha mawe.