Rais wa China Xi Jinping leo Jumatatu Juni 29 amekutana na kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko, mshirika muhimu wa Urusi, huko Beijing, kulingana na vyombo vya habari vya serikali, shirika la habari la AFP limeripoti.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Xi amempokea rais wa Belarusi katika makazi ya kiserikali ya Diaoyutai, televisheni ya serikali ya China,  CCTV, imeripoti. “Uhusiano wa China na Belarus umestahimili mtihani wa changamoto za kimataifa” na “unaingia katika kipindi bora zaidi katika historia yao,” kulingana na taarifa kutoka kwa serikali ya China. 

Xi Jinping amemwambia Lukashenko kwamba nchi zao mbili “zinapaswa kukukusanya rasilimali katika nyanja zote ili kukuza ujenzi” wa mpango mkubwa wa miundombinu wa “Mpango wa Ukanda na Barabara” wa China na kuongeza “ushirikiano wa vitendo,” taarifa hiyo imesema. 

Ziara ya kiongozi huyo wa Belarus inakuja baada ya kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *