Dar es Salaam. Kuna shetani aliyemjaza ujinga Eva bustanini (oldi modeli) Na kuna huyu wa Gen Z shetani wa mitandao (nyu modeli. Wa Eva alifanya tutafute kwa jasho na tuzae kwa uchungu. Wa Gen Z anataka tuishi kifilta filta kwa kila kitu.

Anataka mtu ule chakula kama cha kihoteli hoteli deile. Kuanzia ‘breki fasti’ mpaka dinner. Hivyo ndo vyakula wanavyoposti wehu mitandao. Mateka wa shetani flan ‘ameizing’, achana na yule shetani wa Adam na Eva. Yule hana swaga 

Shetani wa kizazi kipya mwenye makazi mtandaoni. Hufanya mtu akipata msiba asilie bali awaze  juu ya nyumba ya Mabibo. Kama itafaa kwa msiba au akafanyie Mikocheni ulikopanga? Shetani mtandao anakufanya uogope mpaka kivuli chako. 

Shetani mtandao humfanya mtu ashinde ndani kutwa nzima kama hana kitu. ‘Kozi’ akipita mitaani ataonekana tofauti sana na kile anachoonesha mitandaoni siku zote. Watu wamekuwa mateka, watumwa, waumini, wafungwa wa mitandao. 

Wameamua kujipa shida kwenye maisha kwa sababu wanataka kuishi kimtandao. ‘Laifu’ na akili mtandao ukiziendekeza kutaka kushindana nazo, ni sawa sawa na matumizi ya dawa za kulevya. Mitandao ina mateja kibao.

Mateja wa unga kitaa wachache kuliko mateja mtandao. Tofauti ya mateja mitandao na mateja wa unga, wa mitandaoni hawana dhambi. Hawana kasoro wala njaa njaa, sura hazina chunusi na wote weupe. Wamekamilika na wanakosoa kila mtu.

Ukitaka amani na utulivu puuza upuuzi wa mitandao. Kimsingi tofauti ya mitandao na unga ni kwamba unga ni haramu kwa afya ya mwili, akili na kodi kwa serikali. Lakini madhara ni yale yale. Unga na mitandao vyote vinaharibu jamii kwa ukubwa ule ule.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *