Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita imeadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake kwa kushiriki zoezi la upandaji miti katika Shule ya Msingi Bombambili, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhifadhi mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Meneja wa TRA Mkoa wa Geita, Elirehema Kimambo, amesema maadhimisho hayo yamebeba ujumbe wa uwajibikaji kwa jamii, ambapo pamoja na ukusanyaji wa mapato, TRA inaendelea kushiriki shughuli zinazochochea maendeleo endelevu na kulinda mazingira.
Kwa upande wake, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umewahamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kutembelea ofisi za wakala huo ili kupata miche ya miti ya aina mbalimbali kwa ajili ya kuipanda na kuitunza huku Diwani wa Kata ya Kalangalala Reuben Sagayika amewataka Wananchi kutambua ulipaji wa kodi ni sehemu ya kuchochea maendeleo.
(Feed generated with FetchRSS)