#MICHEZO: Kocha wa JKT Tanzania, Hamad Ally, amesema kikosi chake kimekamilisha maandalizi salama kuelekea mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga, akieleza kuwa wanatarajia ushindani mkubwa kutokana na ubora wa wapinzani wao.

Amesisitiza kuwa JKT Tanzania imejiandaa vizuri na ina wachezaji wenye uwezo, huku akiomba kila mmoja awe salama na tayari kwa ajili ya mchezo huo muhimu.

Hamad Ally amesema lengo kuu la timu yake ni kutimiza malengo waliyojiwekea kama JKT Tanzania bila kuangalia mazingira yanayozunguka mchezo huo. Kocha huyo ameeleza kuwa kikosi chake kitaingia uwanjani kikiwa na dhamira ya kupambana na kutoa kiwango bora dhidi ya Yanga katika mechi inayotarajiwa kuhitimisha msimu wa ligi.

Aidha, kocha huyo amewashukuru mashabiki wa JKT Tanzania kwa sapoti waliyoitoa kwa timu katika kipindi chote cha msimu, akiwataka wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao kwenye mchezo huo. Mchezo huo utakaochezwa katika Uwanja wa Meja Isamuhyo unatarajiwa kuwa wa mwisho wa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku ukiwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga katika harakati za kutwaa ubingwa wa ligi.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *