
Makumi ya maelfu ya watu bado hawajulikani walipo baada ya tetemeko la ardhi lililotokea Jumatano ya wiki iliyopita. Wanajeshi wengine wa Marekani wametumwa kurahisisha utoaji wa misaada kwa njia ya anga na kufungua tena bandari ya kimkakati.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Idadi ya vifo kutokana na matetemeko mawili ya ardhi yalilotokea nchini Venezuela imeongezeka tena, alitangaza spika wa Bunge la taifa, Jorge Rodriguez, siku ya Jumapili, Juni 28. “Idadi ya vifo imefikia 1,450 [vifo 1,430 Jumamosi], wanawake na wanaume waliopoteza maisha yao kutokana na majanga ya asili mabaya zaidi ambayo nchi yetu imekumbana nayo katika historia yake yote (…). Idadi ya majengo yaliyoharibiwa au kuanguka imefikia 774, huku 189 yakiporomoka kabisa,” alibainisha.
Timu za uokoaji za kimataifa zinafanya kazi bila kuchoka kuokoa maisha, huku wakazi wenye kukata tamaa wakijaribu kuwakomboa wapendwa wao walionaswa chini ya vifusi na sakafu zilizoanguka za majengo. Katika nchi ambayo uchumi wake umedorora kwa miaka kadhaa, ukosefu wa vifaa vya ujenzi ukiripotiwa nchini huo.
Watu thelathini na watatu, wakiwemo watoto kadhaa, waliokolewa mwishoni mwa wiki ya Juni 27 na 28, alisema rais wa mpito Delcy Rodriguez. “Shughuli za utafutaji na uokoaji zinaendelea. Tumewapata watu wakiwa hai, na kwa hivyo, shughuli hazijasitiishwa. Tunaendelea kuwa na matumaini,” Bi. Rodriguez alisema siku ya Juampili jioni, akiongeza muda wa kufungwa kwa shule kwa wiki nyingine moja.
Umoja wa Mataifa unakadiria idadi ya watu waliotoweka kufikia 50,000, na kuongeza kuwa karibu watu milioni saba wanaaminika kuathiriwa na matetemeko hayo mawili ya ardhi.