Wananchi wa Wilaya ya Mtama mkoani Lindi wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugharamia ujenzi na uboreshaji wa Kituo cha Afya Mtama, mradi ambao umekuwa faraja kwa wakazi wa eneo hilo kwa kusogeza huduma muhimu za afya karibu nao, kupunguza gharama za matibabu pamoja na muda wa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Mradi huo wenye thamani ya Shilingi milioni 580 umewezesha ujenzi wa majengo mbalimbali muhimu ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, jengo la huduma za afya ya uzazi (RCH Clinic) lenye chumba cha upasuaji (theatre), pamoja na jengo la huduma za X-Ray.

Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO), Albert Mpokwa, amesema maboresho hayo yameongeza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Mtama na maeneo jirani.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *