m

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 5

Nani anauza silaha nyingi duniani? Soko la silaha duniani bado liko mikononi mwa mataifa machache yenye nguvu, kutoka bara la Ulaya hadi Asia.

Huku mivutano ya kijiografia ikiongeza duniani na kusababisha vita na migogoro, mahitaji ya vifaa vya kijeshi, kupitia biashara ya silaha, yanazidi kuongezeka katika ulimwengu.

Hapa kuna orodha ya wauzaji 10 wakubwa wa silaha duniani kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti juu ya Amani ya Stockholm (SIPRI), iliyochapishwa Machi 9, 2026.

Marekani 42%

ds

Chanzo cha picha, Getty Images

Marekani inaendelea kukua, ikishikilia nafasi yake kama kiongozi asiye shindika katika soko la silaha. Kulingana na SIPRI, Washington ilisafirisha silaha kwa nchi 99 kati ya 2021 na 2025, zikiwemo 35 barani Ulaya, 18 barani Amerika, 17 barani Afrika, 17 barani Asia-Pasifiki, na 12 mashariki ya Kati.

Kimataifa imechangia 42% (+27% mwaka 2016-2020), kwa mauzo ya nje. Ulaya imekuwa, kwa mara ya kwanza baada ya miongo miwili, mpokeaji mkuu (38%) wa silaha za Marekani, mbele ya Mashariki ya Kati (33%).

Saudi Arabia, ambayo inapokea asilimia 12 ya mauzo ya nje ya Marekani, ndiyo mteja mmoja mkubwa zaidi wa Marekani huko Mashariki ya Kati. Zaidi ya hayo, zaidi ya ndege 460 za kivita za F-35 zinazoelekea Ulaya bado zinasubiri kuwasili.

Ufaransa 9.8%

sx

Chanzo cha picha, Getty Images

Ufaransa inashika nafasi ya pili duniani kwa kipindi cha pili mfululizo, ikisambaza silaha kwa nchi 63. Nafasi hii bila shaka inachangiwa na mafanikio yake katika mauzo ya ndege ya Rafale, ndege ya kivita yenye uwezo mkubwa.

Kimataifa imechangia 9.8% (ikilinganishwa na +21% 2016–2020), karibu 80% ya mauzo ya nje ya Ufaransa huenda katika nchi zilizo nje ya Ulaya, ingawa mauzo ya ndani katika bara hilo yameongezeka kwa kasi (+452%).

Wateja wakuu wa Ufaransa ni India, Misri, Ugiriki, Qatar na Falme za Kiarabu (UAE). Na bado kuna zaidi ya ndege 180 za kivita na meli 16 za kivita zinazosubiri kuwasilishwa.

Urusi 6.8%

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Urusi, ambayo hapo awali ilikuwa muuzaji wa nje wa pili kwa ukubwa duniani, imekumbwa na anguko kubwa la mauzo ya silaha tangu uvamizi wa Ukraine mwaka 2022.

Kimataifa inachangia 6.8% (wakati ilikuwa na 64% 2016-2020), Mahitaji ya ndani ya Urusi yamekuwa makubwa kutokana na vita vya Ukraine.

Shinikizo la Marekani na Ulaya kwa nchi nyingine ili kupunguza ununuzi wa silaha za Urusi pia limechangia kushuka kwa mauzo. Matokeo yake, 74% ya mauzo ya nje yaliyobaki ya Urusi yamejikita katika nchi tatu: India (48%), China (13%), na Belarusi (13%).

Jambo lingine linaloathiri Urusi ni maendeleo ya China na India, katika viwanda vyao vya silaha, na hivyo kupunguza utegemezi wao kwa mshirika huyu.

Ujerumani 5.7%

n

Chanzo cha picha, Getty Images

Ujerumani inaipiku China na kuingia katika nafasi ya 4 duniani, ikichangia asilimia 5.7 ya mauzo ya nje ya silaha.

Berlin inapeleka 24% ya mauzo yake kwenda Ukraine kwa njia ya misaada ya kijeshi na 17% kwa mataifa mengine ya Ulaya. Hata hivyo, zaidi ya nusu ya mauzo yake yanaelekezwa kwa nchi zilizo nje ya bara la Ulaya.

Ujerumani ina utaalamu katika utengenezaji wa nyambizi, vifaru na mifumo ya ulinzi wa anga, miongoni mwa mambo mengine.

China 5.6%

k

Chanzo cha picha, Getty Images

China imeanguka na kupitwa na Ujerumani. Kimataifa inachangia 5.6%, ya mauzo yake ya nje katika masoko machache.

Pakistani ndiyo mteja mkubwa zaidi wa China, ikichukua 47% ya mauzo yake ya nje. Inafuatiwa na Bangladesh, ambayo hupokea 16% ya mauzo ya nje ya China.

Hata hivyo, China imeanzisha mauzo katika masoko ya Afrika na Asia Kusini. Tusubiri tuone itakuwaje.

Italia 4.8

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Italia imeshuhudia kuboreka, ikipanda kutoka nafasi ya 10 hadi ya 6 katika viwango vya dunia. Imepata ongezeko la 157% ikilinganishwa na 2016–2020.

Zaidi ya nusu ya mauzo ya nje ya Italia (59%) yanaelekea Mashariki ya Kati, huku 16% yakienda Asia-Oceania na 13% kwenda Ulaya.

Italia ina wataalamu katika utengenezaji wa helikopta, manowari za saizi ya kati, na ndege za mafunzo.

Israel 4.4%

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Kimataifa inauza 4.4% (ikilinganishwa na 3.1% mwaka 2016-2020), Israeli imefikia hatua muhimu ya kihistoria kwa kuipiku Uingereza kwa mara ya kwanza kimataifa.

Ikiwa na utaalamu katika mifumo ya ulinzi wa anga, ndege zisizo na rubani na teknolojia za ufuatiliaji, Israeli inaaminika sana katika uwanja wa ulinzi wa anga.

Kuna mahitaji makubwa ya kimataifa ya mifumo ya ulinzi wa anga, ambayo inasaidia mauzo yake ya nje. Mauzo yake yameendelea kuongezeka licha ya vita huko Gaza.

Uingereza 3.4%

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Uingereza haijaachwa nyuma, uwezo wake katika utengenezaji wa silaha hutegemea programu za Marekani na Ulaya.

Kimataifa inachangia 3.4%, Uingereza ina utaalamu katika utengenezaji wa meli kubwa za kivita (meli za kubeba ndege, meli za kivita) na ndege za kivita (Typhoon).

Inashirikiana kwa karibu na Marekani na washirika katika Shirika la Mkataba wa Atlantiki Kaskazini (NATO).

Korea Kusini 3.0%

m

Chanzo cha picha, JUNG YEON-JE / AFP

Korea Kusini imejiimarisha kama mmoja wa wauzaji wenye nguvu katika soko la silaha duniani, ikichangia kimataifa 3.0%.

Korea Kusini imepata mafanikio makubwa barani Ulaya, ambapo 46% ya bidhaa zake zinazouzwa nje huenda Poland.

Katika soko la Asia, Korea Kusini hutoa 14% ya mauzo yake nje kwa Ufilipino.

Korea Kusini ina taaluma katika kutengeneza vifaru vya K2, ndege za K9, na ndege za FA-50.

Uhispania 2.3%

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Uhispania imeimarisha nafasi yake katika 10 bora kutokana na ushiriki wake katika miradi ya Ulaya, kama vile Eurofighter na A400M, miradi miwili mikubwa zaidi ya ushirikiano wa kijeshi na viwanda barani Ulaya.

Uhispania ina uwezo katika kuzalisha meli za kivita na magari ya kivita, na inafaidika kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya Ukraine na nchi nyingine za Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *