• Mwanafunzi wa Kidato cha Nne alipatikana amefariki katika Mawego National Polytechnic baada ya mzozo wa kifamilia kuhusu simu ya mkononi
  • Polisi walieleza jinsi tukio hilo lilivyotokea na kuwashauri wazazi na walezi kuzingatia ustawi wa kihisia wa watoto wao
  • Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti mjini Oyugis huku mamlaka zikianzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo

Homa Bay: Mwanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka Kijiji cha Karairo, katika Eneo Bunge la Kabondo Kasipul, amefariki baada ya madai ya mzozo kati yake na wazazi wake.

Mwanafunzi mmoja amefariki baada ya kudaiwa kuwa na ugomvi na wazazi wake.
Mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka Homa Bay afariki baada ya mzozo wa kifamilia. Picha: NPS.
Source: UGC

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17, ambaye ni mwana wa afisa wa polisi, alipatikana amefariki Jumatatu, Juni 29, baada ya kuondoka nyumbani kwao.

Nini kilisababisha kifo cha mwanafunzi wa Homa Bay?

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Rachuonyo Kaskazini, Peter Walah, alithibitisha tukio hilo, huku uchunguzi wa awali ukionyesha lilitokana na mzozo kati ya mwathiriwa na wazazi wake kuhusu simu ya mkononi.

Walah alisema mama wa kijana huyo alidaiwa kumnyang’anya simu baada ya kugundua kuwa matokeo yake ya masomo yalikuwa yameshuka. Polisi walisema uamuzi huo huenda ulimkasirisha.

Pia soma

Homa Bay: Profesa wa Chuo Kikuu cha Maseno Adaiwa Kuuawa Kikatili Kufuatia Mzozo wa Ardhi

Kwa mujibu wa Citizen TV, ripoti ya polisi ilionyesha kuwa kijana huyo alisubiri hadi babake alipoingia kuoga, kisha akachukua bastola yake na kuondoka nyumbani. Baadaye mwanafunzi huyo alipatikana amefariki ndani ya Mawego National Polytechnic, akidaiwa kujipiga risasi.

“Babake ni afisa wa polisi anayefanya kazi katika kaunti ya Meru. Alisubiri baba yake aingie bafuni kisha akaondoka kwa siri akiwa amechukua bastola. Mama yake alienda shuleni kwake na kugundua kuwa matokeo ya mwanawe yalikuwa yameshuka. Akaamua kumnyang’anya simu ya mkononi kama njia ya kumsaidia kuelekeza akili kwenye masomo,” Walah alisema.

Polisi waliwashauri wazazi na walezi kutanguliza ustawi wa kihisia wa watoto wao na kutafuta huduma za ushauri nasaha wanapoona dalili za msongo au huzuni.

Walah alithibitisha kuwa uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea, ikiwa ni pamoja na kubaini kwa nini mwanafunzi huyo alikwenda katika taasisi hiyo kabla ya kifo chake.

Wakati huo huo, mwili wa kijana huyo ulihamishwa hadi katika Chumba cha Kuhifadhi Maiti cha Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Rachuonyo Kusini mjini Oyugis huku uchunguzi ukiendelea pamoja na maandalizi ya mazishi.

Wakenya walivyoitikia tukio la Homa Bay

Nancy Munuhe

“Watoto wetu wamepotea njia imagine na hata kuwakosoa ama kuwapa ushauri, wengine wao hawataki… hawawezi kufanya kila kitu wanachotaka.”

Pia soma

Magazetini Jumatatu, Juni 29: Ripoti ya Siri kwa Ruto Yafichua Mzozo wa Kanja na NPSC

David Onchonga

“Msiba huu wa kusikitisha ni ukumbusho kwamba afya ya akili lazima ichukuliwe kama jambo la dharura katika sekta zote za jamii. Uelewa zaidi, huruma na upatikanaji wa msaada ni muhimu ikiwa tunataka kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu wengi.”

Esther Kimani

“Waaah! Baba yake atajibu maswali mazito sana. Bastola siyo kitu cha kuchezea cha kuachwa ovyo!”

Blessed Suleiman

“Kosa la kwanza ni la baba yake. Kwa nini uache silaha ya serikali mahali ambapo familia yako inaweza kuifikia? Hata kama unaenda chooni, nenda nayo au uwe na sanduku salama nyumbani ambalo hakuna mwingine isipokuwa wewe anaweza kulifungua. Pole kwa familia.”

Mwanafunzi wa Taasisi ya Ufundi ya Thika apatikana amefariki

Katika tukio lingine, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 21, Elizabeth Ngina, alipatikana ameuawa kikatili katika nyumba ya mpenzi wake katika Mtaa wa Kiang’ombe, mjini Thika.

Elizabeth Ngina alipatikana ameuawa kikatili katika nyumba ya mpenzi wake.
Mpenzi wa mwanafunzi wa chuo cha Thika akiongea baada ya kugundua mwili wake nyumbani kwake. Picha: Elizabeth Ngina.
Source: Facebook

Familia yake ilidai mwili wake ulikuwa na majeraha 32 ya kuchomwa kisu huku vidole vyake vikiwa vimekatwa. Mwili huo ulipatikana ukiwa umefichwa chini ya kitanda katika nyumba hiyo ya kukodisha.

Pia soma

Upinzani Wapasuka! Gachagua, Sifuna na vigogo wengine wakwepa maandamano ya Gen Z

Mpenzi wake, ambaye alidai alikuwa hayupo nyumbani, alisema alitumia ufunguo wa akiba kuingia ndani ya nyumba yake, ambayo ilidaiwa kufungwa kutoka ndani. Aligundua mwili huo alipokuwa akijaribu kusukuma beseni chini ya kitanda lakini halikuweza kusogea.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *