- Mshawishi na mwanamitindo wa Colombia, Natalia Villalba, alipatikana amefariki ndani ya sanduku la mizigo katika nyumba ya kifahari ya Airbnb mjini Bogotá baada ya mfanyakazi wa usafi kufanya ugunduzi wa kutisha
- Raia wa Uingereza, Matthew Ashley Foster-Smith, alikamatwa nchini Ecuador baada ya mamlaka za Colombia kumhusisha na kifo cha mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36
- Wachunguzi wanadai mshukiwa alimshambulia Villalba, akauficha mwili wake ndani ya sanduku la mizigo, akaharibu ushahidi katika eneo la tukio na kutoroka kabla ya kukamatwa
Mwanamitindo na mshawishi maarufu, Natalia Villalba, amepatikana amefariki ndani ya sanduku la mizigo katika nyumba ya kifahari ya kukodisha kwa muda mfupi ya Airbnb mjini Bogotá.

Source: Facebook
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 anaripotiwa alikuwa akiishi katika nyumba hiyo iliyoko El Chicó, kitongoji cha kifahari katika mji mkuu wa Colombia, kuanzia Juni 3 na alitarajiwa kuondoka Juni 21.
Hata hivyo, mkasa ulitokea baada ya mfanyakazi wa usafi kuingia kwenye nyumba hiyo Juni 22 na kudaiwa kugundua mwili wa Villalba ukiwa umefichwa ndani ya sanduku la mizigo lililoachwa ndani ya bafu lililokuwa wazi.

Pia soma
Miezi 3 Baada ya Shambulio la Tindikali, Mary Claire Afunguka na Kufichua Ujumbe wa Kutisha
Ni nani aliyekamatwa kuhusiana na kifo cha Natalia Villalba?
Mamlaka za Colombia zimemkamata raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 46, Matthew Ashley Foster-Smith, kuhusiana na kifo cha mshawishi huyo.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Colombia, wachunguzi wanaamini mshukiwa aliingia katika nyumba aliyokuwa akiishi Villalba akiwa peke yake na kudaiwa kumshambulia kabla ya kuweka mwili wake ndani ya sanduku la mizigo.
Mamlaka pia zinadai kuwa alijaribu kuficha uhalifu huo kwa kuharibu ushahidi katika eneo la tukio kabla ya kutoroka.
Mshukiwa alifuatiliwa na kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Quito nchini Ecuador mnamo Juni 26 kufuatia operesheni ya pamoja iliyohusisha vyombo vya usalama vya Colombia, Ecuador na Uingereza.
Meya wa Bogotá, Carlos F. Galán, alipongeza ushirikiano huo akisema kuwa wote wanaohusika na uhalifu jijini humo watafikishwa mbele ya sheria.
Kabla ya kukamatwa kwake, Foster-Smith alikanusha kuhusika na kifo cha Villalba katika mahojiano na gazeti la The Sun.
Alidai alikuwa akitazama mechi ya Kombe la Dunia ya England kabla ya kwenda katika kituo cha ununuzi na baadaye kurejea kuendelea kutazama soka.

Pia soma
Msichana wa Chuo cha Thika, 21, Apatikana Amekufa Nyumbani kwa Mpenzi Akiwa na Majeraha 32 ya Visu
Licha ya maelezo yake, taarifa zinaonyesha kuwa mshukiwa huyo ana rekodi ya makosa ya jinai nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa BBC, Smith aliwahi kutumikia kifungo cha zaidi ya miaka miwili gerezani kwa makosa ya ufuatiliaji wa kero (stalking). Baada ya kuachiliwa, aliwekwa chini ya amri ya kuzuia ufuatiliaji iliyomtaka kuripoti mara kwa mara mahali alipo kwa polisi na kumzuia kuwasiliana na waathiriwa wake.
Uchunguzi kuhusu kifo cha Villalba unaendelea huku mamlaka zikiendelea kubaini matukio yaliyopelekea kuuawa kwa mshawishi huyo.
Tazama video hapa chini:
Nini kilimpata Constance Githinji?
Katika habari nyingine za kusikitisha, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Murang’a mwenye umri wa miaka 22, Constance Githinji, alifariki baada ya kudaiwa kuanguka kutoka ghorofa ya sita ya jengo la makazi huko Kileleshwa.
Taarifa zinaonyesha kuwa Constance alikuwa amesafiri kwenda Nairobi baada ya kukutana na Tony Odhiambo mwenye umri wa miaka 33 kupitia jukwaa maarufu la uchumba kabla ya tukio hilo la kusikitisha.

Source: UGC
Uchunguzi ulipoendelea, video iliyosambazwa na mmoja wa marafiki zake ikimuonyesha mwanafunzi huyo akijiandaa katika saluni saa chache kabla ya kifo chake ilisambaa mitandaoni, jambo lililowaacha Wakenya wengi wakiwa na huzuni na kudai haki itendeke.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke
