Mazungumzo yasiyokuwa ya ana kwa ana kati ya wajumbe wa Iran na Marekani, yamemalizika jijini Doha, bila ya kuonekana kwa matumaini ya kuelewana kuhusu mkataba wa amani wa kudumu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti za ndani kutoka kwenye mazungumzo hayo, zinasema, wajumbe kutoka nchi hizo mbili walitoa muda mwingi kujadili hatima ya eneo la mlango wa Bahari ya Hormuz na Marekani kuachia fedha za Iran zilizozuiwa.

Wizara ya Mambo ya nje ya Qatar kupitia ukurasa wake wa X, imesema hatua chanya imepigwa kwenye mazungumzo hayo, ambayo yanaendeleza makubaliano yaliyoafikiwa mwezi Juni na kumaliza vita.

Naye rais wa Marekani Donald Trump amesema, mazungumzo hayo yanalenga kuhakikisha kuwa uwezo wa Iran kuendelea na mpango wake wa nyuklia unapungua.

Iran nayo inasema itawasiliana na Marekani, kujadili baadhi ya maeneo ambayo yamekiukwa kwenye mkataba wa kusitisha vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *