Cristiano Ronaldo amesema kuwa hajafanya uamuzi wowote kuhusu hatima yake katika timu hiyo, kauli ambayo inaonyesha wazi anainga kile kilichosemwa na dada yake Katia Aveiro.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 41, amesema kwamba suala la kustaafu au kutostaafu kuichezea Ureno, hajalifanyia kazi kwa vile huu sio wakati sahihi wa kufanya hivyo.

Na badala yake, Ronaldo amesema kuwa anachofikiria hivi sasa ni kusaidia Ureno ifanye vizuri katika Fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazoendelea katika nchi za Mexico, Canada na Marekani.

“Hatima yangu sio kitu cha muhimu hivi sasa. Nitakuwa na muda baada ya kushinda au kupoteza, wa kuongea na familia yangu na kufanya uamuzi bora.

“Sifanyi uamuzi katika wakati ambao mambo yamepamba moto. Kwa sasa mambo yanafanyika kwa utulivu. Ni suala la kufurahia wakati tuliopo,” alisema Ronaldo.

Juzi, Katia Aveiro alinukuliwa akisema kwamba mashindano haya ya Kombe la Dunia mwaka huu ni nafasi ya mwisho kwa Ronaldo kuitumikia timu ya taifa ya Ureno kwani hana mpango wa kuendelea kuichezea baada ya hapo.

Muda mfupi baada ya kauli hiyo ya dada yake, Ronaldo aliiongoza Ureno kutinga hatua ya 16 baada ya kuifungia bao moja katika ushindi wa mabao 2-1 ambao timu hiyo ilipata dhidi ya Croatia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *