Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma,  aliyehusika katika kashfa nyingi za ufisadi – alitembelea hekalu nchini India mwishoni mwa mwezi Juni na alionekana pamoja na mmoja wa ndugu wa Gupta, anayejulikana kwa jukumu lake la kuiteka serikali wakati wa Jacob Zuma alipokuwa madarakani. Ingawa chama cha MK, chama kipya cha rais Jacob Zuma aliyeondolewa madarakani, kinamtetea, kikielezea kama safari ya kibinafsi iliyoidhinishwa, serikali inaona ziara hiyo kama aibu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Valentin Hugues

Ziara hii inaturudisha nyuma zaidi ya miaka kumi, hadi wakati wa uongozi wa Zuma, kilele cha ufisadi ulioenea, ndugu wa Gupta walishutumiwa kuwa wahusika wa kuu wa ufisadi huu uliokithiri.

Kwa hivyo, picha hii ya hivi majuzi ya Jacob Zuma pamoja na Ajay Gupta ni dharau kwa mujibu wa Waziri katika Ofisi ya Rais Khumbudzo Ntshavheni. “Inatia wasiwasi sana kwamba rais wa zamani anaweza, kwa uwazi na bila huzuni yoyote, kuwashushia heshima Waafrika Kusini ambao walipoteza pesa nyingi kwa sababu ya ndugu wa Gupta. Na anaongeza kwamba anataka kuiongoza nchi hii tena! Hilo linaonyesha wazi ni mtu wa aina gani, na ni jukumu la Waafrika Kusini kuamua wenyewe.

Ndugu wa Gupta bado wanatafutwa na Afrika Kusini

Kwa sababu katika ziara hii nchini India, rais wa zamani, ambaye sasa ni kiongozi wa chama cha MK, mpinzani wa chama cha ANC, pia alionyesha nia yake kuwania kiti cha urais. Mnamo mwaka 2018, alilazimika kuondoka madarakani. Siku ya kujiuzulu kwake, msako wa polisi ulifanyika katika ofisi za ndugu wa Gupta – washirika wa rais aliyetimuliwa, ambao wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa euro bilioni kadhaa. Wafanyabiashara hao wenye asili ya Kihindi walitoroka nchi hii na bado wanasakwa na Pretoria.

Kufuatia mkutano huu nchini India, Jacob Zuma anaweza kupoteza marupurupu yake kama rais wa zamani, ambayo yanajumuisha kurejeshewa gharama zake za usafiri nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *