Nchini Madagascar, rais wa mpito Michaël Randrianirina amezungumzia suala la ndege zisizo na rubani siku ya Jumamosi, Julai 5, 2026. Kulingana na mamlaka, ndege mbili zisizo na rubani zilizotiliwa shaka ziliruka juu ya msafara wa rais Ijumaa jioni huko Antananarivo. Mkuu wa serikali ya mpito alilaani hili kama jaribio la kusababisha hofu na kuwataka raia wa Madagascar kuwaripoti wale waliohusika.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Antananarivo, Guilhem Fabry

Milio ya risasi ilisikika Ijumaa jioni katika kitongoji cha kifahari cha Ivandry, wakati msafara wa rais ukipita, ilizua wasiwasi miongoni mwa wakazi waliorekodi na kushiriki tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii. Walinzi wa rais walifyatua “risasi” katika jaribio la kuziangusha ndege hizo zisizo na rubani, lakini hawakufanikiwa.

Mkuu wa nchi aliweza kurudi nyumbani kwa usalama. Kutoka kitengo cha Capsat, ambapo ametpka, Michaël Randrianirina alihutubia tukio hilo Jumamosi. “Kwa siku mbili mfululizo, ndege zisizo na rubani zilifuata msafara wa rais. Ndege ya kwanza ilionekana siku ya Alhamisi jioni, lakini haikuweza kushambuliwa. Jana usiku, tukio kama hilo lilitokea tena, kwa hivyo tulionyesha kwamba tulikuwa tayari kulipiza kisasi kwa sababu sisi si vibaraka. Watu hawa wanataka kusababisha hofu ili kuonyesha ulimwengu kwamba hali nchini Madagascar si shwari.””

Ndege zisizo na rubani zilikuwa juu sana angani na hazingeweza kudondshwa, kulingana na maelezo kutoka kwa ofisi ya rais. “Ninatoa wito kwa kuwafichua wahusika kwani watu hawa wanaorusha ndege zisizo na rubani wako katika vitongoji vyenu. Tuambie ni nani aliyezirusha! Jeshi limekuwa likitumia kifaa cha kuzuia ndege zisizo na rubani tangu asubuhi ya leo. Ninaishukuru Urusi kwa kifaa hiki, lakini haitoshi. Tutapata zaidi ili kubaini  wahusika wa hali hii.”

Mkuu wa nchi, ambaye mara kwa mara anadai kuwa analngwa na vitisho, anaweza kutegemea msaada wa Moscow. Wakufunzi kutoka kundi la kijeshi la Urusi la Africa Corps wamekuwa wakiwafunza wanajeshi wa Madagascar, wakiwemo kikisi cha walinzi wa rais, kwa miezi sita iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *