Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amelaani vitisho vya hivi karibuni vya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen, akisema kuwa vinafichua kufeli Riyadh kisiasa na kijeshi pamoja na kushindwa kwake kusambaratisha mapambano ya Yemen licha ya nchi hiyo kuathirikwa kwa miaka mingi na vita na mzingiro.

Mohammed al-Farah amepinga taarifa ya karibuni ya muungano wa Saudia na kuitaja kuwa “kashfa ya kisiasa na simulizi iliyopitwa na wakati.”

Amesema kuwa muungano huo umebaki na vitisho pekee baada ya miaka 11 ya vita, mzingiro, na operesheni za kijeshi ambazo zote zimeshindwa kufikia malengo yao waliyokusudia.

Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen ameeleza kuwa Saudi Arabia imetumia mabilioni ya dola kwa mamluki na vibaraka huku yenyewe ikikabiliwa na vikwazo vya kisiasa na kupoteza sifa kimataifa.

“Riyadh inaendelea kujificha nyuma ya kile kinachojulikana kama Ramani ya Amani ili kurefusha vita badala ya kusatifa suluhu ya kweli ya kisaisa. Kauli ya muungano wa Saudia  inakisi namna muungano huo ulivyochanganyikiwa kisiasa na kijeshimkabala wa kampeni ya Sana’aa ya kukabiliana na mzingiro dhidi yake,” ameeleza Mohammed al-Farah Afisa wa ngazi ya juu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen.

Inafaa kuashiria kuwa mapema leo Jumapili muungano unaoongozwa naSaudi Arabia umetishia kutoa jibu kali kwa hatua yoyote ya kuilenga nchi hiyo ya kifalme.

Muungano wa Saudia umetoa vitisho hivyo saa chache baada ya vikosi vya ulinzi vya vya Yemen kusema kuwa vitavishambulia viwanja vya ndege vya Saudi Arabia na vituo vya kimkakati vya ardhi na baharini ikiwa Riyadh itaendelea kukiuka anga ya Yemen au kuanzisha shambulio jipya la kijeshi dhidi ya Yemen.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *