Kampuni kubwa ya utengenezaji wa bidhaa za kielektroniki ya JIUZHOU kutoka China imeipongeza Azam Media Limited kwa uwekezaji wake pamoja na ubora wa utayarishaji wa maudhui yake.
Pongezi hizo zimetolewa baada ya ujumbe wa JIUZHOU kutembelea makao makuu ya Azam Media Limited yaliyopo Tabata Dar es Salaam, ambapo pia walionesha nia ya kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu unaolenga kukuza biashara na teknolojia katika sekta ya vyombo vya habari na mawasiliano.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya ugeni huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited Divisheni ya Teknolojia na Miundombinu, Ahmed Abdallah amesema ujio wa kampuni hiyo unatokana na uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya pande hizo mbili.
Amesema Azam Media itaendelea kushirikiana na washirika wake wa kimataifa katika kuimarisha ubunifu na utoaji wa huduma bora kwa watazamaji.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)