Mamia kwa maelfu ya raia wa Iran wakiwemo wageni, hivi leo wanatarajiwa kujitokeza katika barabara ambazo msafara uliobeba mwili wa aliyekuwa kiongozi wa juu wa taifa hilo, Ayatollah Ali Khameni, utapita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baada ya raia kupata nafasi ya kutoa heshima katika msikiti mkubwa zaidi wa Grand Mosalla mjini Tehran, waandaaji wa shughuli hiyo wanasema safari ya mazishi itachukua saa 10 hadi 12, mamlaka zikijaribu kuzuia maafa yaliyotokea wakati wa mazishi ya mtangulizi wake.

Katika mazishi ya mtangulizi wake, Ayatollah Ruhollah Khomeini mwaka 1989, zaidi ya watu milioni 10 walijitokeza ambapo 10 walipoteza maisha na wengine zaidi ya elfu 1 kujeruhiwa baada ya kutokea mkanyagano.

Mpaka sasa haijafahamika ni kwa kiasi gani raia wataruhusiwa kusogelea msafara wake ili kuepuka kilichotokea mwaka 89 ambapo mamlaka zililazimika kutumia ndege kusafirisha mwili wa Khomeini.

Katika shughuli ya hapo jana, watoto watatu wa Kahamenei walihudhiria ibada ya mazishi isipokuwa mrithi wake Mojtaba Khamanei, ambaye tangu aripotiwe ujeruhiwa katika mashambulio ya Februari 28, hajawahi kuonekana hadharani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *