• Winnie Odinga amefunguka kuhusu miezi minane iliyofuata baada ya kifo cha Raila Odinga, akieleza kwa nini imekuwa kipindi kigumu zaidi maishani mwake
  • Alikumbuka mzigo wa kihisia wa kutangaza kifo cha babake na kutoa hotuba ya heshima katika mazishi yake ya kitaifa huku bado akijaribu kukabiliana na majonzi
  • Winnie pia alidai alishuhudia urithi wa kisiasa ambao Raila aliujenga kwa miongo kadhaa ukivunjwa na watu ambao alikuwa amewaamini kuulinda

Binti wa mwisho wa Raila Odinga, Winnie Odinga, amefunguka kuhusu changamoto za kihisia alizokumbana nazo katika miezi iliyofuata baada ya kifo cha babake mwaka jana.

Winnie Odinga akizungumza kwenye mazishi ya kitaifa ya Raila Odinga.
Winnie Odinga alifunguka kuhusu hali ya kihisia ya miezi kadhaa kufuatia kifo cha babake, Raila Odinga. Picha: Winnie Odinga, Raila Odinga.
Source: Facebook

Mwanasiasa huyo mkongwe alifariki dunia baada ya kuanguka alipokuwa akitembea asubuhi nchini India, alikokuwa amesafiri kutafuta matibabu maalumu.

Winnie alikuwa miongoni mwa wanafamilia waliomsindikiza katika safari hiyo, na baadaye akapewa jukumu gumu la kutangaza habari za kifo chake.

Kwa nini kifo cha Raila Odinga kimekuwa kigumu kwa Winnie?

Baada ya kifo cha babake, Winnie alimheshimu kwa njia mbalimbali, ikiwemo kutoa hotuba iliyogusa wengi yenye maneno:

Pia soma

Magazetini: Ruto amvaa Gachagua, azima madai kuwa ndiye aliyemletea kura za Mlima Kenya 2022

“Mfalme amefariki, lakini taji na liendelee kuishi.”

Miezi kadhaa baadaye, mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) alitafakari kuhusu athari kubwa ambayo msiba huo umeacha katika maisha yake.

Akizungumza katika hafla ya hivi karibuni, Winnie alisema miezi minane iliyopita imekuwa kipindi kigumu zaidi kuwahi kukipitia.

Alieleza kuwa muda mfupi kabla ya msiba huo alikuwa akicheka, akizungumza na kumkumbatia babake, lakini ghafla akajikuta akirejea Kenya ndani ya ndege iliyokuwa ikisafirisha mwili wake.

Winnie alisema hakupata hata nafasi ya kuomboleza ipasavyo kabla ya kuombwa azungumzie hadharani mtu ambaye alikuwa amemtoa sehemu kubwa ya maisha yake kumhudumia.

“Niliambiwa nizungumzie mtu ambaye nilijitolea maisha yangu kwake. Hakuna aliyefikiria au kujua kwamba wakati huo nilichokuwa nikifikiria ni kwamba muda mfupi uliopita nilikuwa naye tukizungumza, tukicheka, tukikumbatiana na nikihisi uwepo wake. Mara moja baada ya hapo nikaambiwa, ‘Fanya hili, na lazima ulifanye na ulifanye kikamilifu.'”

Winnie Odinga akiwa amebeba kofia ya kifahari ya babake ya fedora.
Winnie Odinga alifunguka kuhusu changamoto za kihisia alizopitia kufuatia kifo cha babake. Picha: Musalia Mudavadi.
Source: Getty Images

Winnie alisema nini kuhusu urithi wa Raila?

Kwa mujibu wa Winnie, maumivu yake yaliongezeka aliposhuhudia kile alichokitaja kuwa kuvunjwa kwa urithi wa kisiasa wa babake na watu ambao alikuwa amewaamini kuulinda.

Pia soma

Ndindi Nyoro adokeza kuhusu mipango yake ya kisiasa baada ya kula hu kwa William Ruto

Alikumbuka kuwa alipozungumzia suala hilo wakati huo, alikosolewa kwa namna alivyosema badala ya hoja alizokuwa ameibua.

“Nilihisi maumivu makubwa sana, na nilizungumza, lakini wakasema sikuwa na heshima. Nilizungumza kwa sababu nilijua nilichokuwa nikisema kilikuwa sahihi, lakini mjadala ukaishia kwenye namna nilivyosema nilichosema, hivyo nikajiondoa na nikahuzunika. Walitaka kunidhibiti na, kwa kiwango fulani, walifanikiwa.”

Winnie alisema baadaye alitambua kuwa ukosoaji huo haukuhusu tu maneno yake.

“Watu kama mimi hawapaswi kusema mambo niliyokuwa nikisema kwa watu kama wao.”

Licha ya changamoto hizo, Winnie alisema ameendelea kukumbatia safari yake ya uponyaji.

“Maombolezo hayaji na mwongozo wa matumizi. Wakati mwingine unatarajiwa kutabasamu huku ukiwa umebeba mzigo ambao hakuna anayeuona. Kuongoza kabla hujapata nafasi ya kupona. Kuwa imara wakati bado unajaribu kuelewa kilichotokea.

Hii ndiyo simulizi yangu, si ya kupoteza pekee, bali pia ya ustahimilivu. Na kama itamkumbusha mtu yeyote kwamba uponyaji si safari ya mstari ulionyooka, basi kushiriki simulizi hili kulikuwa na thamani.”

Tazama video hapa chini:

Je, Winnie Odinga anamiliki The BrickHouse Counsel?

TUKO.co.ke pia iliangazia taarifa kuhusu kampuni isiyojulikana sana ya Winnie, The BrickHouse Counsel, ambayo imekuwa na ushawishi mkubwa katika siasa barani Afrika na kwingineko.

Pia soma

“Naumwa na tumbo”: Maneno ya mwisho ya mwalimu Mkenya aliyefariki akiwa Thailand yahuzunisha

Ikiwa na orodha ya wateja inayojumuisha marais sita pamoja na klabu ya soka ya Uingereza, Everton, kampuni hiyo ni mfano wa nguvu ya mawasiliano ya kimkakati katika kuunda mtazamo wa umma na simulizi za kisiasa.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *