
Ripoti hiyo inaonesha kuwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, karibu watu bilioni moja wamepata maji salama ya kunywa, bilioni 1.2 huduma bora za usafi wa mazingira, maambukizi mapya ya VVU yamepungua kwa asilimia 30, huku asilimia 92 ya watu duniani sasa wakipata umeme.
Pamoja na hayo
Hata hivyo, mtu mmoja kati ya kumi bado anaishi katika umaskini uliokithiri, watu bilioni 2.3 wanakabiliwa na uhaba wa chakula, watoto na vijana milioni 273 hawapo shuleni, na maendeleo katika karibu nusu ya malengo 139 yanayofuatiliwa ni ya polepole mno.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu kuhusu Maendeleo Endelevu, HLPF, jijini New York, Marekani Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed ametoa wito wa mageuzi katika mfumo wa fedha duniani ili kusaidia nchi kupata nafuu ya madeni na ufadhili wa muda mrefu kwa miradi ya maendeleo.
Naye Rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Jamii (ECOSOC), Lok Bahadur Thapa, amesema Ajenda ya 2030 bado ni ahadi ya pamoja kwa dunia, akisisitiza kuwa sasa ni wakati wa kubadili ahadi kuwa vitendo.
Soma zaidi hapa.