Nchini Kenya Polisi wamesema hawataruhusu maandamano yaliopangwa kufanyika leo Jumanne jijini Nairobi kuadhimisha siku ya saba saba kuendelea.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hadi tukichapisha taarifa hii, usalama ulikuwa umeimarishwa jijini Nairobi, magari yanayoingia katikati wa jiji hilo yakikaguliwa na maofisa wa usalama.

Maandamano yamekuwa yakifanyika kila tarehe 7 ya kila mwaka kuadhimisha siku ambayo Wakenya walijitokeza mwaka wa 1990 kushinikiza kurejeshwa kwa demokrasia ya vyama vingi wakati wa utawala wa hayati Rais Daniel arap Moi. Tangu wakati huo, siku hii imekuwa ikijulikana kama saba saba.

Katika kipindi cha miaka miwili iliopita, waandamanaji wamekuwa wakitumia siku ya saba saba kuandamana dhidi ya utawala wa Rais William Ruto, ambaye wanamtuhumu kwa ufisadi, kuharibika kwa uchumi pamoja na kuwaruhusu polisi kutumia nguvu zaidi.

Karibia watu 38 waliuawa kote nchini wakati mamia ya wengine wakikamatwa wakati wa maandamano ya Julai 7 mwaka uliopita kwa mujibu wa takwimu za mashirika ya kiraia.

Polisi wameimarisha usalama zaidi katika maeneo mbalimbali ya jiji, wakipiga marufuku maandamano ya mwaka huu.

Maofisa wa usalama wanasema hakupokea notisi ya maandamano ya leo Jumanne lakini waliopanga maandamano haya wanasema walitoa taarifa kwa muda kuhusu mipango yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *