Balozi Mavura anasema, “Kiswahili kwa asili yake ni lugha ya amani. Ni vigumu kugombana na lugha ya Kiswahili.”

Anaendelea kufafanua kuwa lugha ya Kiswahili ina maneno machache ya kugombana lakini ina maneno mengi ya maridhiano na anaongeza akisema, “kwa ajili hiyo ni lugha ambayo imetsaidia sana katika eneo letu la Aftika Mashariki kwa sababu (pia) ni lugha ya biashara kwa asili yake. Ni lugha ya watu waliokutana kutoka katika maeneo mbalimbali. Ilikuwa lugha ya kuwaunganisha watu. Kwa hiyo Kiswahili ni lugha daraja na si lugha ya kutenganisha watu.

Mfuko wa kubebea vitu vya bluu wenye maandishi na nembo umewekwa kwenye meza ya mbao nje.

UN/ Stella Vuzo Mfuko huu mahsusi umeandaliwa kutangaza jinsi tasnia ya habari inavyochangia katika kueneza na kukuza lugha ya Kiswahili duniani.

Bwana Togolani anasema katika jumuiya za kiuchumi ambazo zimefanikiwa sana barani Afrika ni Jumuiya ya Afrika Mashariki, “na moja ya siri yake ni kwa sababu inatumia lugha ya Kiswahili.”

Wazungumzao hawagombani

Balozi Togolani Mavura anaamini katika msemo wa Waswahili usemao ‘Wazungumzao hawagombani’ na kwa hivyo anasema, “kwa hiyo tunaamini kwamba kadiri Kiswahili kitakavyopanuka kwenda kwenye maeneo mengine ndivyo amani itapanuka kwenda kwenye maeneo mengi na ndio maana lugha ya Kiswahili inatumika katika majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *