Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema ufafanuzi uliotolewa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) umeondoa kwa kiwango kikubwa mkanganyiko uliokuwa umejitokeza kuhusu sababu za mabadiliko ya bei za mafuta nchini, huku ukiweka wazi mchakato mzima wa uagizaji na uundaji wa bei hizo.
Akizungumza baada ya kikao kati ya wahariri, Wizara ya Nishati na TPDC, Balile alisema mkutano huo ulifanyika kufuatia maswali mengi kutoka kwa wananchi kuhusu sababu zilizopelekea athari za mabadiliko ya soko la mafuta duniani kuonekana kwenye bei za mafuta nchini baada ya muda badala ya kuonekana mara moja.
(Feed generated with FetchRSS)