Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umejipanga kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kufanikisha lengo la Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia unaolenga kuboresha afya za wananchi, kulinda mazingira na kupunguza matumizi ya nishati zisizo salama.
Akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia za Nishati Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, amesema REA itaendelea kutoa elimu kwa wananchi pamoja na ruzuku kwa wenye nia ya kutumia majiko ya nishati safi lakini wanakabiliwa na changamoto ya uwezo wa kifedha.
Naye mkurugenzi wa uchunguzi wa bidhaa na mazingirana kutoka mamlaka ya maabala ya mkemia mkuu wa serikali Shimo Peter amewataka wananchi kutembelea banda lao ili kupata elimu ya kazi ya mamlaka ya maabala ya mkemia mkuu wa serikali .
Kwa upande wake katibu tawala mkoa wa kigoma hasan rugwa amesema uwepo kwa maonyesho ya sabasaba unaongeza wawekezaji katika mkoa wa kigoma
Kwa upande wake afisa namba moja kutoka bodi ya wabunifu na wakadiliaji majenzi Sunday Njovu amesema ni wakati sasa wanatekeleza miradi ya ujenzi ni kushirikisha bodi ili kupata majengo yenye ubora na kwa bei halisia.
(Feed generated with FetchRSS)