
Akihutubia hii leo Julai 8 Baraza la IMO huko London, Uingereza makao makuu ya shirika hilo, Dominguez amesihi wamiliki wa meli na mamlaka husika kutotumia mlango huo kwa sasa hadi pale usalama wa vyombo na wafanyakazi utakapokuwa umepatiwa hakikisho.
Takribani mabaharia wamekwama ndani ya meli kwenye mlango huo tangu mwezi Aprili hadi sasa wakishindwa kuondoka eneo hilo kwa hofu ya mashambulizi. Hivyo Dominguez amesihi pande husika kujizuia na mashambulizi ili kuwezesha meli kuondoka kwa usalama.