
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametia saini marekebisho ya Katiba, yanayoongoza muda wake wa kusalia madarakani hadi mwaka 2030.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Msemaji wa serikali Nick Mangwana amethibitisha hatua hiyo ya rais Mnangagwa, inayobadilisha hali ya kisiasa katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika.
Kwa mujibu wa marekebisho hayo, muhula wa rais na wabunge kukaa madarakani kabla ya kufanyika kwa uchaguzi umeongezwa hadi miaka saba, kutoka miaka mitano.
Aidha, kwa mujibu wa sheria hiyo mpya, rais atakuwa anachaguliwa na wabunge wala sio wananchi moja kwa moja, kama ilivyokuwa hapo awali.
Rais Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 83, alikuwa aondoke madarakani mwaka 2028, lakini kwa sheria hii mpya, atasalia kuwa kiongozi wa nchi hiyo hadi mwaka 2030.
Wapinzani nchini Zimbabwe walipinga mabadiliko hayo, waliyosema ni mbinu ya Mnangagwa, kusalia madarakani kwa muda mrefu kama alivyokuwa mtangulizi wake, Hayati Robert Mugabe aliyeongoza kwa karibu miaka 40.