
Unyanyasaji wa kingono unaendelea kutumiwa kama silaha ya kivita, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ripoti hiyo iliyotolewa siku ya Jumatano, Julai tarehe nane, imeeleza kuwa unyanyasaji huo unatumiwa kama njia ya kulipiza kisasi dhidi ya raia wa kawaida, mbali na wizi na utekakaji unaotekelezwa na makundi yenye silaha.
Tume ya haki za binadamu inasema, unyanaysaji wa kingono unatekelezwa pia wakati wa operesheni za kijeshi katika maeneo yenye utovu wa usalama, Mashariki mwa DRC.
Wanajeshi wa serikali FARDC wanatuhumiwa kuhusika na ubakaji wa wanawake na wasichana 15,vikosi vya kigeni visa sita huku kundi la M23 likiropotiwa kuwabaka wanawake 12, sawa na wanajihadi wa ADF na waasi wa Mai Mai.
Katika kipindi cha mwezi mmoja, visa 37 vya unyanaysaji ikiwemo ubakaji umeripotiwa kwenye maeneo yenye vita, huku waathiriwa wakiwa wanawake na wasichana 16.
Jimbo la Kivu Kaskazini linaongoza kwa visa hivyo, ambapo asilimia 60 vimeripotiwa, huku Ituri na Kivu Kusini zikifuata.