Kila inapofika misimu ya baridi, baadhi ya wananchi mkoani Njombe huuchukulia kama kipindi cha kawaida cha mwaka, huku wengine wakitumia fursa hiyo kuendesha biashara zinazohitajika zaidi wakati wa hali hiyo ya hewa.
Hata hivyo, kwa baadhi ya wakazi, msimu wa baridi huambatana na changamoto zinazogusa afya, elimu na maisha ya kila siku.
Azam News inaangazia hali hiyo wakati tayari Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kuhusu ongezeko la baridi katika maeneo mbalimbali nchini.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)