Kwa zaidi ya miaka 40, wakazi wa Kata ya Kiponzelo mkoani Iringa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kupata huduma za upasuaji, hali iliyowaweka katika mazingira magumu hasa wajawazito waliolazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

Baada ya kutembea zaidi ya kilomita 70 kufuata huduma za upasuaji, sasa matumaini mapya yamepatikana baada ya kukamilika kwa jengo la upasuaji lenye thamani ya shilingi milioni 124, lililojengwa kwa ushirikiano kati ya jamii na World Vision Tanzania.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *