• Sheria ya Fedha 2026 imeondoa tarehe ya mwisho ya Juni 30 ya kuwasilisha marejesho ya kodi ya mapato kwa KRA, na kuweka tarehe mpya kwa makundi tofauti ya walipa kodi
  • Wakenya wanaolipwa mishahara na kukatwa kodi kupitia mfumo wa PAYE sasa watawasilisha marejesho yao ya kila mwaka miezi miwili mapema kuliko ilivyokuwa awali, huku wanaowasilisha nil returns pia wakipewa tarehe mpya
  • Tarehe hizi mpya zitaanza kutumika Januari 1, 2027, na zitatumika kwa mara ya kwanza kwa marejesho ya mwaka wa mapato wa 2026

Serikali ya Kenya imeondoa tarehe ya muda mrefu ya Juni 30 ya kuwasilisha marejesho ya kodi ya mapato na kuanzisha ratiba mpya zenye tarehe tofauti chini ya Sheria ya Fedha 2026, hatua itakayowaathiri wafanyakazi wanaolipwa mishahara, kampuni na watu wanaowasilisha nil returns.

Maafisa wa mapato wa KRA wakiwa kazini.
Sheria ya Fedha ya 2026 ilianzisha makataa mapya ya kurejesha kodi. Picha: KRA.
Source: Twitter

Mabadiliko hayo yataanza kutekelezwa Januari 1, 2027, na yatatumika kwa mara ya kwanza kwa marejesho yanayohusu mwaka wa mapato wa 2026, hivyo walipa kodi wataanza kuwasilisha marejesho yao kwa mfumo mpya kuanzia mwaka 2027.

Pia soma

Morara Kebaso: Kiasi cha karo anacholipa mfanyabiashara kumsomesha mwanawe katika Woodcreek School

Tarehe Mpya za Kuwasilisha Marejesho ya Kodi KRA ni Zipi?

Wafanyakazi wanaolipwa mishahara ambao mapato yao yote yanakatwa kodi kupitia mfumo wa Pay As You Earn (PAYE) watahitajika kuwasilisha marejesho yao ya kodi ya kila mwaka kufikia Aprili 30, miezi miwili mapema kuliko tarehe ya awali ya Juni 30.

Wakenya wanaowasilisha nil returns, kundi linalojumuisha wasio na ajira, wanafunzi, wamiliki wa PIN zisizotumika na watu wasio na mapato yanayotozwa kodi, sasa watalazimika kuwasilisha marejesho yao kufikia Januari 31 kila mwaka.

Hivi majuzi Adan Mohammed alichukua wadhifa wa bosi wa KRA.
Bosi wa KRA Adan Mohammed (c) na maafisa wengine. Picha: KRA.
Source: Twitter

Kampuni zinazowasilisha marejesho ya tathmini binafsi (self-assessment returns) zitakuwa na muda hadi mwezi wa sita baada ya mwisho wa mwaka husika wa mapato kuwasilisha marejesho yao, huku watu binafsi wanaowasilisha tathmini binafsi wakitakiwa kufanya hivyo kufikia mwezi wa nne baada ya mwisho wa mwaka wa mapato.

Waajiri bado watatakiwa kutimiza wajibu wao wa kila mwezi wa kuwasilisha na kulipa kodi ya PAYE, licha ya mabadiliko ya tarehe za kuwasilisha marejesho ya kila mwaka.

Sheria ya Fedha 2026 pia imefanyia marekebisho Kifungu cha 52(1) cha Sheria ya Kodi ya Mapato, kwa kuongeza muda ambao mlipa kodi anatakiwa kujibu ombi la maandishi kutoka kwa Kamishna kuhusu marejesho ya kodi, kutoka siku 30 hadi miezi minne baada ya mwisho wa mwaka wa mapato.

Pia soma

Safari ya mwisho ya Tony Ndiema: Familia yatangaza tarehe na mipango ya mazishi

Mabadiliko Haya Yana Athari Gani?

Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA) inatarajiwa kunufaika na muda huu mpya wa mapema kwa walipa kodi binafsi, kwani kuwasilishwa kwa marejesho mapema kutairuhusu kuthibitisha haraka wale wasiokuwa na wajibu wa kulipa kodi na kuweka rekodi za uzingatiaji wa sheria zikiwa za kisasa mwaka mzima.

Hata hivyo, mabadiliko haya yatawaongezea walipa kodi binafsi shinikizo la kukamilisha rekodi zao za kifedha na nyaraka zinazohitajika kwa haraka zaidi mara mwaka wa mapato unapomalizika.

Tarehe mpya ya Aprili kwa wafanyakazi wa PAYE, hasa, inapunguza muda ambao hapo awali ulikuwepo wa kukusanya na kuwasilisha nyaraka muhimu.

Marekebisho hayo yanaoanisha ratiba mpya na zile zilizowekwa tayari chini ya Sheria ya Taratibu za Kodi (Tax Procedures Act) kuhusu tathmini zilizoandaliwa mapema (pre-populated assessments), hatua ambayo serikali imesema itaboresha ufanisi wa kiutawala katika mamlaka ya ukusanyaji wa mapato.

Sheria ya Fedha 2026 Imeleta Mabadiliko Gani Mengine?

Katika habari zinazohusiana, Sheria ya Fedha 2026 imerejesha mpango wa msamaha wa kodi (tax amnesty), ambao utaendelea hadi Desemba 31, 2026.

Pia soma

Video ya askari akipiga sherehe na mpenzi wake kabla ya kudaiwa kumtupa kutoka ghorofa ya 6 yaibuka

KRA ilieleza kuwa walipa kodi watakaolipa deni lao kuu la kodi kwa mkupuo watahitimu moja kwa moja kusamehewa adhabu na riba.

Msamaha huo unahusu tu madeni ya kodi yaliyotokana na wajibu uliokuwepo hadi Desemba 31, 2025. Kwa wale wasioweza kulipa kwa mkupuo mmoja, mamlaka hiyo imetoa fursa ya kuomba mpango maalumu wa malipo kwa awamu.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *