Mwili wa mfanyakazi wa Azam Media, Daniel Laizer aliyekuwa akihudumu katika idara ya uratibu vipindi kama mfasiri wa lugha, umeagwa leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Machimbo Tabata jijini Dar es Salaam.

Ibada hiyo ya kuaga imehudhuriwa na ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi pamoja na viongozi wa Kampuni ya Azam Media, kabla ya mwili wa marehemu kusafirishwa kwenda kijiji cha Sunya wilayani Kiteto mkoani Manyara kwa ajili ya mazishi.

Akizungumza wakati wa ibada hiyo, mwakilishi wa Azam Media, Amani Zacharia amesema Daniel Laizer ataendelea kukumbukwa kwa umahiri wake katika ufasiri wa lugha, ikiwemo kutafsiri tamthilia mbalimbali zilizokuwa zikirusha kupitia Azam Two pamoja na kuendesha vipindi vya lugha ya Kiingereza kama The Magazine.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *