Nkasi yapata kituo cha afya cha bil 1.8/-Nkasi yapata kituo cha afya cha bil 1.8/-

RUKWA: Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi kupitia ujenzi wa miundombinu ya kisasa, ambapo Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Juma Zuberi Homera, amezindua Kituo cha Afya Nkasi kilichojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 1.8 katika Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa kituo hicho, Mganga Mfawidhi George Hemed alisema huduma zilianza kutolewa Agosti 2023 baada ya kukamilika kwa majengo saba, na hadi sasa zaidi ya wananchi 90,000 wamepata huduma mbalimbali za matibabu, huku wanawake 197 wakifanyiwa upasuaji wa uzazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Homera alisema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuwekeza katika sekta ya afya ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi karibu na makazi yao.

Aidha, aliwataka watumishi wa afya kutoa huduma kwa weledi na kuzingatia maelekezo ya Serikali.

Kwa upande wao, wananchi wa Nkasi waliishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya, wakisema kituo hicho kimepunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu, hususan huduma za uzazi na dharura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *