PART ONE
Wahenga wanasema, ‘Tembea uone’. Lakini pia Asiyesafiri haoni mengi na wapo wanaongeza kuwa ‘Elimu haina mwisho’
Methali hizi zina mana kubwa katika maisha ya kawaida, ziikichochea wanajamii kutokaa sehemu moja tu na kwamba wakisafiri na kutembelea maeneo mbalimbali watapata maarifa, uzoefu na uelewa mpana wa maisha.
Pia, ufundisha kwamba mtu ujifunza mengi kwa kuona na kushuhudia mambo mwenyewe kuliko kusikia simulizi za wengine pekee kwani endapo utapata wasaa wa kutembelea mikoa mbalimbali ya Tanzania, utagundua tamaduni nyingi tofauti.
Moja ya vivutio hivyo ni hifadhi za Taifa. Tanzania imebarikiwa kuwa na hIfadhi mbalimbali na moja wapo ni HIfadhi ya Taifa ya Saadan iliyopo mashariki mwa Tanzania, kati ya mikoa ya Pwani na Tanga. Ni hifadhi ya kipekee kwa sababu ndiyo hifadhi pekee nchini ambapo wanyamapori na Bahari ya Hindi hukutana wakiwamo tembo, simba, twiga, nyati, viboko, mamba na aina mbalimbali za swala.
Hata hivyo, ukifika Saadan hutoona wanyama pekee bali kuna utalii wa safari za boti kwenye Mto Wami, ambapo unaweza kuona viboko, mamba na ndege wengi pamoja na fukwe za Bahari ya Hindi zenye mandhari ya kuvutia wakiwamo ndege wa aina mbalimbali.
Cha kipee zaidi ni utalii wa miti. Ndiyo namaanisha Miti hasaa. Ukifika Saadan utakutana na Miti mbalimbali ambayo wazee wazamani walikuwa wakitumia kwa ajili ya masuala ya mila na desturi za Pwani.
Kati ya miti hiyo ni ‘MTI MAPENZI’ unaopatikana ndani ya HIfadhi ya Taifa ya Saadan ukiwa na namaajabu makubwa.
Jina “Mti wa Mapenzi” limetokana zaidi na simulizi na desturi za watalii na waongozaji wa safari, ambao huutaja kama sehemu ya kimahaba ambako ina aminika ukichuma tawi la mti huo na kumchapa nao mtu unayempenda basi lazima akufuate.
Wenyeji wanasema vijana wengi walitumia mti huo mpaka kufikia hatua ya kuchumbia na kuoa. Lakini kwa MTI MAPENZI’ sharti lazima uwe unampenda kweli mwanamke au mwanaume huyo lkn pia wakati unachuma na kwenda kumchapa nao uliyemkusudia lazima unuie.
✍️✍️ Tausi Mbowe
(Feed generated with FetchRSS)