INTERNATlONAL SWIM CAMP 2026 | North Coast Swimming Club kwa kushirikiana na Prime Sports Agency wameandaa msimu wa pili wa kambi maalum ya kuogelea iitwayo International Swim Camp 2026, inayofanyika katika Shule ya DIS Campus, Mbweni jijini-Dar es Salaam ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kiushindani waogeleaji.

Kambi hiyo iliyoanza Julai 1 inatarajiwa kuhitimishwa Julai 15 ikiwa imewakutanisha zaidi ya waogeleaji 60 kutoka mataifa mbalimbali makocha pamoja na wataalamu wa kimataifa wanaotoa mafunzo na kubadilishana uzoefu.

Mkurugenzi Mkuu wa North Coast Swimming Club, Lameck Borega amesema kambi hiyo itasaidia kuinua kiwango cha mchezo wa kuogelea nchini kwa kuwapa waogeleaji mafunzo ya kisasa yatakayowawezesha kushindana katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

Naye kocha wa North Coast Swimming Club, Khalid Rushaka amesema waogeleaji wanapata mbinu mpya za mazoezi na kuimarisha uwezo wao wa ushindani.

Huku mmoja wa wazazi wa washiriki wa kambi hiyo, Marien Chisonga amewahamasisha wazazi kuwapa watoto nafasi ya kushiriki katika kambi hizi ili kukuza vipaji, nidhamu na kujiamini.

#Swimming #AzamSports

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *