.

Chanzo cha picha, Reuters

Marekani imesema imeanzisha wimbi jipya la mashambulizi
dhidi ya Iran baada ya Iran kushambulia meli iliyokuwa ikipita katika Mlango wa
Bahari wa Hormuz.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC)
limetangaza kufungwa kwa njia hiyo muhimu ya baharini hadi itakapotolewa
taarifa nyingine, huku likionya kuhusu hatua kali dhidi ya kile lilichokiita “uchokozi” wa Marekani, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.

Saa chache baada ya mashambulizi ya Marekani, IRGC ilidai
kuwa imelenga kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Jordan. Wakati huo huo, Falme
za Kiarabu (UAE), Qatar na Bahrain ziliripoti kuchukua hatua za kukabiliana na
makombora na ndege zisizo na rubani zilizorushwa kutoka Iran.

Mvutano huo unafuatia matukio ya mapema wiki hii ambapo meli
tatu za kibiashara za kubeba mafuta zilishambuliwa, hali iliyosababisha
mashambulizi ya kulipizana kisasi kati ya Marekani na Iran.

Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) ilisema
imeanzisha duru ya tatu ya mashambulizi wiki hii baada ya IRGC kushambulia “waziwazi” meli yenye usajili wa Cyprus, MV GFS Galaxy,
iliyokuwa ikivuka Mlango wa Bahari wa Hormuz.

Kwa mujibu wa CENTCOM, meli hiyo iliharibiwa vibaya katika
chumba cha injini na haikuweza kuendelea na safari yake. Aidha, mfanyakazi
mmoja wa kiraia wa meli hiyo anaripotiwa kutojulikana alipo.

Shirika la Uingereza la UK Maritime Trade Operations (UKMTO)
limesema lilifahamishwa na mamlaka za kijeshi kuwa wafanyakazi wa meli
walilazimika kuiacha baada ya kushambuliwa na kuanza kutumia boti ya kujiokoa.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, CENTCOM
ilisema Iran ilipewa fursa nyingine ya kuonyesha kwamba inazingatia makubaliano
ya Maelewano baada ya kuwajibishwa kwa mashambulizi ya awali dhidi ya meli za
kibiashara, lakini “imeshindwa kufanya hivyo kwa mara nyingine.”

Soma Zaidi Hapa:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *