
Kiungo wa kati Jayden Adams, ambaye alishiriki michuano ya Kombe la Dunia la 2026 akiichezea timu yake ya Afrika Kusini, , Bafana Bafana amefariki ghafla siku ya Jumamosi, Julai 11, akiwa na umri wa miaka 25, Waziri wa Michezo wa Afrika Kusini ametangaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Simanzi, vilio na huzuni vimetawala ulimwengu wa mpira wa miguu. Jayden Adams alifariki baada ya kushiriki baadhi ya michezo ya Kombe la Dunia. “Nilipatawa na mshtuko mkubwa niliposikia kuhusu kifo cha Jayden Adams,” alisema Waziri wa Michezo wa Afrika Kusini Gayton McKenzie katika taarifa, bila kutaja chanzo cha kifo hicho, ambacho “hakijathibitishwa bado.” “Soka la Afrika Kusini limepoteza mmoja wa vipaji vyake vichanga,” aliongeza.
“Hii ni siku mbaya sana kwa soka nchini Afrika Kusini,” waziri huyo aliongeza. “Kipaji kama Jaden hakiji kila siku. Alivunja rekodi. Alijitolea kwa ajili ya wengine. Alikuwa bado kijana na mtu mwenye uelewa, sijui nielezee nini.”
Rais wa FIFA Gianni Infantino alisema “amehuzunishwa sana” na kifo cha Jayden Adams, akitoa “rambirambi zake kwa niaba ya FIFA na jumuiya ya kimataifa ya mpira wa miguu kwa familia yake, marafiki, na wachezaji wenzake.”
Polisi walitangaza kuwa wameanzisha uchunguzi baada ya mwili wa mwanamume mwenye umri wa miaka 25 kupatikana Jumamosi asubuhi katika nyumba moja huko Schotschekloof, kitongoji kinachopatikana katikati mwa Cape Town, ili kubaini mazingira ya kifo chake. Siku ya Jumamosi, jamaa na wafuasi walikusanyika kuzunguka nyumba yake huko Cape Town, ambapo alipatikana amefariki. Chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana, na familia bado haijazugumza chochote.