MLANDEGE inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), imetangaza kuachana na mshambuliaji wake, Mussa Hassan ‘Mbappe’ huku ikimtakia kheri katika safari yake mpya.

Katika taarifa iliyotolewa na timu hiyo, ilimpongeza kwa hatua yake mpya ya kujiunga na Singida Black Stars inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Tunakupongeza kwa hatua yako mpya ya kujiunga na Singida, tunakutakia mafanikio makubwa katika kila hatua ya safari yako,” imeeleza taarifa hiyo.

Pia, ilitoa pongezi kwa mchezaji huyo kwa kujitoa, kupambana na kuipa klabu kila alichokuwanacho huku ikieleza mchango wake umeacha alama ambayo itabaki kuwa sehemu ya historia yao.

Mwanaspoti ilimtafuta mshambuliaji huyo kutaka kujua undani wa taarifa ya kujiunga na Singila.

Mbappe alisema, Mkataba baina yake na Mlandege umeisha hivyo anasubiria mambo yakamilike atatoa taarifa kwa mashabiki wake.

“Mkataba wa kuitumikia Mlandege umeisha ila kwa upande wa Singida bado mambo hayajakamilika ndio maana nimekaa kimya,” amesemaMbappe

Mshambuliaji huyo alimaliza msimu wa 2025-2026 akifunga mabao tisa katika Ligi Kuu Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *