Hati rasmi kutoka ofisi ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa Baraza Kuu la Sudan, imevuja kwa vyombo vya habari. Hati hiyo inaonyesha kuwepo kwa mpango wa kisiasa ambao al-Burhan anafanyia kazi ili jeshi liendelea kuwa madarakani wakati wa kipindi cha mpito cha miaka mitano. Mwishoni mwa kipindi hiki, uchaguzi mkuu utafanyika.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na hati iliyoandikwa katikati ya mwezi Juni, Jenerali al-Burhan anaandaa maono ya kisiasa na kimkakati kwa Sudan. Hati hiyo inapendekeza kuundwa kwa serikali ya mpito itakayoundwa na  watu wenye utaalamu wa hali ya juu kwa muhula wa miaka mitano, ambayo itaandaa mazungumzo ya kitaifa ili kuwezesha uchaguzi.

Hata hivyo, watu ambao hawana hati yoyote nchini Sudan ndio watakaoshiriki katika mazungumzo haya kati ya Wasudan.” Jambo hili tayari limesemwa mara kadhaa na Jenerali al-Burhan na timu yake. Hati hiyo inakataa uwezekano wowote wa kupitisha maazimio ya mazungumzo yanayofanyika nje ya nchi. Inamaanisha kwamba serikali ya Sudan inapinga suluhisho lolote linalotolewa kutoka nje.

Hata hivyo, jeshi bado halijajibu mpango uliopendekezwa mwezi Juni na Mjumbe Maalum wa Rais wa Marekani kwa Afrika, Masaad Boulos. Kutokana na shinikizo la Marekani, jeshi hilo limerudia madai yake ya kuondoka kwa wanamgambo wa vikosi  vya Msada wa Haraka (RSF) kutoka mijini kabla ya majadiliano yoyote. Hoja muhimu katika makubaliano ya Jeddah yaliyosainiwa na pande hizo mbili zinazopigana.

Uungwaji mkono wa Riyadh

Katika mpango wake, al-Burhan anategemea uungwaji mkono wa Saudi Arabia, lakini pia ule wa Uturuki, ambayo alizuru hivi karibuni.

Kulingana na wataalamu kadhaa, hati hiyo inaonyesha mradi wa kisiasa unaolenga kufafanua upya aina ya nguvu baada ya vita na kusambaza upya vituo vya kufanya maamuzi ndani ya serikali. Waangalizi wanahofia kwamba kufuata mipango hii kwa upande mmoja kunaweza kuzidisha nafasi za kufikia suluhu kamili ya kisiasa, kurefusha vita, na kuchelewesha kupatikana kwa makubaliano ya kitaifa ambayo yangerejesha utulivu nchini Sudan.

Kama ukumbusho, jeshi la Sudan lilifanya mapinduzi mnamo mwezi Oktoba 2021 dhidi ya serikali ya mpito iliyokuwa ikiongozwa na raia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *