
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ukaguzi wa jeshi la polisi la kitaifa umebaini makosa mengi. Kati ya faili 158,000 zilizochunguzwa, karibu 40% zilionekana kuwa za kutiliwa shaka. Kwa serikali, suala hilo pia ni la kifedha: kasoro hizi zinaweza kugharimu zaidi ya dola milioni 230 kwa mwaka.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa
Maafisa wasiofanya kazi, maafisa wa polisi wanaodhaniwa kuwa wa uaongo au nyaraka zenye upungufu: ukaguzi wa awali wa polisi wa kitaifa wa Kongo ulibainisha faili 63,817 za kipaumbele zinazohitaji ukaguzi wa kina. Kulingana na serikali, makosa haya yanaweza kuwakilisha hasara ya kati ya dola milioni 8.3 na dola19.4 kwa mwezi, au hadi dola milioni 233 kwa mwaka ikiwa hakuna kitakachofanyika.
Mamlaka sasa inataka kufadhili mpango mkubwa wa utambuzi wa kibiometriki na utoaji wa kadi kwa maafisa wa polisi ili kudhibiti vyema viwango vya wafanyakazi na mishahara.
Lakini ufichuzi huu pia unaibua wasiwasi wa usalama. Mashirika ya kiraia yanasema kwamba nchi hii tayari ina takriban afisa mmoja wa polisi kwa kila wakazi 700, uwiano unaoonekana kuwa hautoshi. Hata hivyo, serikali inapanga kuajiri maafisa wapya 90,000 tu kwa kipindi cha miaka mitano.
Kulingana na vyanzo kadhaa vya polisi, jambo la wafanyakazi hewa linatokana na miaka mingi ya uajiri uliojaa mapungufu, mapendekezo, na madai ya ubadhirifu wa mishahara. Baadhi vyanzo ndani ya jeshi la polisi vinabaini kwamba kurejea kwa muda kwa malipo ya mishahara kutawezesha ukaguzi unaoendelea.