Kesi dhidi ya aliyekuwa daktari nchini Rwanda Eugene Rwamucyo anayetuhumiwa kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994 ,ambayo imekuwa ikiendelea Paris, inaingia kwenye hatua za mwisho.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwezi Oktoba mwaka 2024 ,mahakama ya Paris ilimhukumu daktari huyo aliye na uraia wa Ufaransa, kifungo cha miaka 27 jela kwa kuhusika kwenye mauaji hayo ya kimbari .
Tangu uamuzi huo, amekuwa akibadilisha mfumo wa kujitetea na hoja za mwisho zinawasilishwa wiki hii huku uamuzi mwingine ukitarajiwa kutolewa Ijumaa hii ambapo sasa anakabiliwa na kifungo cha maisha iwapo atashindwa kwenye kesi hiyo.
Awali alikuwa na mawakili wawili lakini kwenye awamu huu ,amewaajiri mawakili wapya saba na msimamo wake kuwa hana hatia ,haujabadilika,licha ya kuwa ushahidi kwa kiasi kikubwa uko kinyume chake.
Baadhi ya makosa dhidi yake ni uchochezi wa mauaji ,kufuatia hotuba yake ya Mei 14 mwaka 1994 alipokuwa daktari na mwalimu ,mauaji ya majeruhi na kushiriki kuzika miili kwenye makaburi ya halaiki.
Rwamucyo aliwasili Ufaransa 1999 na akapewa kibali cha kuishi ,kuendelea na elimu na kutekeleza wajibu wa udaktari ila akakamatwa mwaka 2010 lakini kesi yake imekuwa ikiendelea kwa kasi ndogo.