
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,Mbunge wa Kigoma Mjini Revocatus Chipando maarufu Baba Levo amesema ujenzi wa reli hiyo unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 15,000, hatua itakayosaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa wananchi wa eneo hilo.
Amesema uwekaji wa jiwe la msingi utafanyika Julai 20, 2026, mjini Kigoma, ambapo unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na kupambwa na burudani kutoka kwa wasanii wenye asili ya Kigoma, akiwemo Nasibu Abdul maarufu Diamond Platnumz na Ali Kiba.
Chipando amesema mradi wa SGR unatarajiwa kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa Kigoma kwa kuboresha usafirishaji wa watu na mizigo, kuongeza fursa za biashara na kuvutia uwekezaji katika mkoa huo. SOMA: Ujenzi SGR Tanga-Arusha-Musoma wahojiwa bungeni