
Marekani imetangaza siku ya Jumatatu Julai 13, 2026 mashambulizi makubwa ya kidiplomasia dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), hasimu wake mkuu, inayotuhumiwa “kuwatishia” Wamarekani, huku akiahidi vikwazo vipya na kuwataka washirika wake kujiondoa kwenye mahakama hiyo.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Tunapozungumza, ICC na washirika wake wanapigana vita dhidi ya nchi yetu, si kwa risasi au makombora, bali kwa sheria, mikataba, na nguvu ya kile kinachoitwa ‘sheria ya kimataifa,'” alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio katika ujumbe wa video kwenye mtandao wa kijamii wa X, makala iliyochapishwa katika Gazeti la Wall Street Journal, na katika taarifa kwa vyombo vya habari.
“Hatari inayotokana na mahakama hii ya kimataifa imeongezeka tu. Leo, inatishia kila kipengele cha mfumo wetu wa kisiasa na kisheria,” aliongezaa. Alisema pia kwamba “ikiwa tutasalia kimya, sote tutakuwa chini ya udhibiti wa majaji wa kigeni kwenye umbali wa maelfu ya maili, tukiwa katika hatari ya mara kwa mara ya kushtakiwa, au hata kufungwa, kwa kile kinachoitwa uhalifu wa kutetea nchi yao wenyewe.”
Nia ya kuitenga Mahakama
Wizara ya Mambo ya Nje ilisema inazingatia “hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na marufuku ya usafiri, kufutwa kwa visa, vikwazo vilivyoongezeka dhidi ya ICC na mashirika yanayohusiana, na shinikizo la kidiplomasia kwa nchi zingine kujiondoa kutoka ICC,” kulingana na afisa mmoja akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina. “Wito huu unalenga kushawishi nchi ambazo kwa sasa ni wanachama wa Mkataba wa Roma kujiondoa kutoka ICC na kusitisha usaidizi wowote wa kifedha kwa Mahakama,” alisema.
Hata hivyo, Washington inatoa wito kwa nchi ambazo, kama Marekani, si wanachama wa Mkataba wa Roma kuhamasisha mitandao yao ya kidiplomasia kuchukua hatua kama hizo, ikisema kwamba “hakuna chaguo la kidiplomasia linaloweza kuepukika katika kampeni hii ya kuondoa tishio linalotolewa na ICC kwa Wamarekani.”
Kulipiza kisasi kwa uchunguzi dhidi ya Israel
Uhusiano kati ya utawala wa Trump na ICC, ambayo iko Hague, ni mgumu sana, na majaji kadhaa wa mahakama hiyo, akiwemo mwendesha mashtaka mkuu, tayari wanakabiliwa na vikwazo. Vikwazo hivi vinawakataza majaji kuingia Marekani na kuzuia miamala yoyote ya mali isiyohamishika au fedha nao katika nchi hii yenye uchumi mkubwa zaidi duniani.
Vikwazo hivi kwa kiasi kikubwa ni jibu la uchunguzi uliofanywa na ICC dhidi ya Israel, mshirika wa Marekani. Hasa, mahakama ilitoa hati za kukamatwa mwaka wa 2024 dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Uadui wa Washington dhidi ya ICC si wa pekee kwa utawala wa Trump: serikali za awali zilizoongozwa na chama cha Democratic pia ziliikosoa Mahakama hiyo.
Majaji watatu wa ICC waliochukuliwa vikwazo na utawala wa Trump waliwasilisha kesi mwezi Juni dhidi ya rais na maafisa kadhaa wakuu wa Marekani, wakisema kwamba hatua zilizochukuliwa dhidi yao zilikuwa kinyume cha sheria. Katika malalamiko yaliyowasilishwa New York, jaji kutoka Canada Kimberly Prost, jaji kutoka Uganda Solomy Balungi Bossa, na jaji kutoka Benin Reine Adélaïde Sophie Alapini-Gansou walidai kwamba vikwazo hivi vilikusudiwa “kutoa shinikizo mpya.” Mbali na Donald Trump, kesi hiyo pia inamtaja Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na Waziri wa Fedha Scott Bessent.
ICC iliyoanzishwa mwaka wa 2002, inawashtaki watu binafsi wanaoshutumiwa kwa ukatili mbaya zaidi, kama vile uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na mauaji ya kimbari. Israel wala Marekani si mshiriki wa mkataba wa kimataifa ulioanzisha ICC, wala Urusi, ambayo rais wake, Vladimir Putin, amekuwa chini ya kibali cha kukamatwa tangu mwezi Machi 2023.