Vyanzo vya kijeshi vya tovuti ya Open Source Intelligence (OSINT) vimetoa picha zinazoonyesha kiwango kikubwa cha uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya hivi karibuni ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya shabaha nyeti na za kimkakati za Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

Picha zilizosambazwa na vyanzo hivyo siku ya Jumapili zilihusu taswira za satelaiti zilizopatikana kutoka maeneo yaliyolengwa nchini Jordan, Qatar, Bahrain na Kuwait.

Shabaha mbili zilitambuliwa kuwa ni jengo la kuegeshea  droni aina ya MQ-4C Triton katika Kituo cha Anga cha Prince Hassan nchini Jordan, ambalo lilionekana kuharibiwa kabisa kufuatia shambulio hilo la kulipiza kisasi, pamoja na jengo jingine kama hilo katika Kituo cha Anga cha al-Udeid nchini Qatar, ambacho ni kituo kikubwa zaidi cha Jeshi la Anga la Marekani  katika eneo hilo.

Picha nyingine ilionyesha athari za shambulio la kombora dhidi ya ghala la kuhifadhia vifaa katika makao makuu ya Kikosi cha Tano cha Wanamaji wa Marekani nchini Bahrain.

Taswira nyingine pia ilionyesha moto ukiwaka katika kambi ambayo Marekani imekuwa ikitumia kuzindua mashambulizi kwa kutumia mfumo wa makombora wa HIMARS (High Mobility Artillery Rocket System).

Marekani imetekeleza ukiukaji mwingi dhidi ya ardhi ya Iran tangu Aprili 7, wakati Rais wa Marekani Donald Trump alipotangaza kwa upande mmoja usitishaji mapigano katika duru ya karibuni ya mashambulizi makubwa ya pamoja ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.

Ukiukaji huo uliendelea hata baada ya Washington na Tehran kusaini hati ya makubaliano ya maelewano iliyopatanishwa na Pakistan, ambayo kifungu chake cha kwanza kinaeleza wazi ulazima wa kusitishwa kwa uchokozi katika medani zote.

Jeshi la Iran limekuwa likitoa majibu makali kwa kila tukio la ukiukaji, ikiwa ni pamoja na yale yaliyofanyika kwa kuunga mkono harakati haramu za vyombo vya majini katika Lango la Hormuz.

Mapema mwezi huu, Jamhuri ya Kiislamu ilipanua mkakati wake wa kulipiza kisasi kujibu ukiukaji huo, ikiahidi kulenga shabaha za adui kwa uwiano usiopungua mbili kwa moja; yaani, kwa kila shabaha ya Iran itakayopigwa, angalau shabaha mbili za adui zitashambuliwa kwa kujibu.

Zaidi ya hayo, Iran imefunga Lango la Hormuz kwa usafiri wote wa majini, na ikaweka sharti kwamba kufunguliwa kwake tena kutategemea kusitishwa kwa uingiliaji wa kijeshi wa Marekani katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *