Jeshi la Colombia liliwaachilia huru watu 39 siku ya Jumanne, Julai 14, ambao walikuwa wametekwa nyara na ELN, kundi kubwa zaidi la wapiganaji wa msituni nchini humo ambalo bado linaendesha harakati zake, afisa mmoja amesema. Wanajeshi wawili wa Colombia waliuawa.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kundi la waasi la ELN liliwakamata watu hawa – akiwemo mtoto mdogo – barabarani katika eneo la mbali la Chocó, ambapo kundi hilo lenye silaha lina idadi kubwa ya waoiganaji wake. “Wananchi wetu 39 wamepata uhuru wao,” alitangaza Jenerali Hugo López, akibainisha kuwa wanajeshi wawili waliuawa wakati wa operesheni ya uokoaji. Chanzo cha kijeshi hapo awali kililambia shirika la habari la AFP, kwa sharti la kutotajwa jina, kwamba wote waliotekwa nyara walikuwa raia waliokuwa wakisafiri kwa basi.

Askari wawili wa Colombia waliuawa wakati wa operesheni ya uokoaji. “Wakati wa operesheni hii, yenye lengo la kulinda maisha na uhuru wa Wacolombia, wanajeshi wetu wenye ujuzi zaidi Elibert Ducuara Mosquera na Jean Carlos Vallejo Vargas waliuawa wakitimiza wajibu wao mtakatifu zaidi kwa taifa,” alisema kamanda mkuu wa vikosi vya jeshi. “Msaada na mchango wao kwa taifa utaheshimiwa na haitasahaulika kamwe.” 

Kundi la waasi lenye zaidi ya wapiganaji 6,800

ELN ambayo ilianzishwa tangu mwaka wa 1964 haikushiriki katika makubaliano ya kihistoria ya amani ambayo, miaka kumi iliyopita, yalifanya waasi wengi wa zamani wa FARC kuweka silaha zao chini na kurejea katika maisha ya kiraia. Kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa Wakfu wa fondation Ideas para la Paz, iliyochapishwa mwezi Januari, ELN ilikuwa na wapiganaji 6,810 mwaka wa 2025, ongezeko la 9% ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mbali na kuendesha harakati zake huko Chocó, kundi hili la waasi lina ushawishi kaskazini-mashariki na kusini-magharibi mwa nchi.

Serikali ya Rais anayeondoka Gustavo Petro, mbabe wa zamani kivita kutoka  waasi wa kundi la M-19 lililovunjika, alijaribu bila mafanikio kufanya mazungumzo ya amani na ELN alipoingia madarakani mwaka wa 2022. Mpango huo ulivunjika bila mafanikio mwezi Januari 2025, wakati mapigano kati ya wapinzani wa ELN na FARC yaligharimu maisha ya watu zaidi ya mia moja na makumi ya kusababisha maelfu ya watu kuyatoroka makazi yao huko Catatumbo, eneo linalopakana na Venezuela.

Utekaji nyara ulikumba kampeni ya uchaguzi wa urais

Makundi ya watu wenyeyamekuwa mengi nchini Colombia katika kipindi cha miaka minne iliyopita, kulingana na wataalamu. Nchini Colombia, utekaji nyara mikononi mwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya ni jambo la kawaida, ambalo lilikumba kampeni ya uchaguzi wa urais mwaka huu.

Rais mteule nchini Colombia, Abelardo de la Espriella (kutoka mrego wa kulia wenye msimamo mkali), ameahidi kuimarisha sera za usalama na kufanya mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya waasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *