.

Chanzo cha picha, Hannes Klostermann/ Ocean Image Bank

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 5

Wanadamu wana mengi yanayofanana na papa kuliko ilivyodhaniwa?

Papa ni miongoni mwa wanyama wawindaji asili duniani.

Wao na papa wa awali walinusurika kutoweka kwa wingi kwa awamu zote tano, ikiwa ni Pamoja na kutoweka kwa Permian-Triassic, au “Maafa makubwa”.

Tukio hili la hali ya hewa mbaya liliangamiza viumbe vingi duniani, ikiwa ni pamoja na takriban 90% ya viumbe vya baharini.Lakini papa waliendelea kuishi.

Leo wanapatikana katika karibu kila sehemu ya Bahari, na baada ya mamia ya mamilioni ya miaka ya mageuzi, wamekuza sifa za kushangaza.

Haya hapa maajabu nane ya papa usioyafahamu.

1.Papa hufanya hisabati.

Ingawa papa mara nyingi hufikiriwa kuwa wanyama wanaowinda bila kujali, walio na sifa ya kujali tu njaa yao, sayansi inaonyesha kwamba ni werevu na wanafunzi wazuri. Wanaweza kutofautisha kati ya sauti tofauti, pamoja na mifumo tofauti ya kufikirika na maumbo ya kijiometri yenye rangi.

Katika jaribio moja maarufu, papa wachanga wa mianzi ya kijivu walionyeshwa kukumbuka taarifa kuhusu maumbo na maumbo yasio halisia kwa macho kwa karibu mwaka mmoja.

Pia wanaweza kufanya hisabati ya msingi, wakionyesha tofauti kati ya kiasi kama vile tatu na tano, na nne na saba ila si kiasi kinachokaribiana kama nne na tano.

2. Papa ni waraibu wa mziki wa jazz

Kwa papa aina ya Port Jackson, muziki sio mziki kama hauna mvuto wa mawimbi ya mziki yani ‘swing’.

Aina hii ya papa, ambao hupatikana Australia na kuishi sehemu za chini ya maji, walipewa mtihani wa kuogelea kuelekea eneo maalum ndani ya tangi lao wakati muziki unapopigwa ili wapate chakula kama zawadi.

Utafiti uliofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Macquarie jijini Sydney ulionyesha kuwa papa hao walipendelea eneo hilo la kulia chakula wakati muziki wa ‘jazz’ ukipigwa, lakini hawakuweza kuhusisha eneo hilo na muziki wa ‘classical’.

“Ilikuwa dhahiri kuwa papa hao walijua wanapaswa kufanya jambo fulani wakati muziki wa ‘classical’ unapopigwa, lakini hawakuweza kutambua kuwa walipaswa kwenda eneo tofauti,” alisema mtafiti Culum Brown alipokuwa akizungumza na wanahabari.

.

Chanzo cha picha, Jayne Jenkins/Ocean Image Bank

3. Papa wana vitovu

Ingawa papa wengi hutaga mayai, baadhi yao wakiwemo papa aina ya ng’ombe na nyundo, hubeba watoto wao kwenye mfuko wa uzazi na kuwalisha kupitia kitovu, kama wanadamu.

Hii ndiyo sababu, kwa wiki chache au miezi michache baada ya kuzaliwa, watoto hawa huwa na vitovuni vya tumboni hadi kovu vinapopona.

Papa wengine hawatagi mayai wala kulea watoto wao tumboni kama mamalia. viinitete au Watoto wao hukua kwenye mayai ambayo huanguliwa wakiwa bado ndani ya mama. Watoto hawa pia huzaliwa wakiwa hai. Papa wa spiny dogfish huzaliwa hivi, kwa mfano, baada ya ujauzito ambao unaweza kudumu hadi miaka miwili.

4. Watoto wa papa hula wenzao wakiwa tumboni mwa mama yao

Watoto wa papa aina ya *sand tiger* hujikuta katika mapambano ya kuishi tangu hatua za awali kabisa,wakiwa bado ndani ya tumbo la mama yao.

Papa jike wa aina hii huwa na mifuko miwili ya uzazi, na kila mfuko unaweza kubeba hadi watoto watano. Hata hivyo, viinitete hivyo hula ndugu zao hadi kubaki na mtoto mmoja tu.

Hali hii inajulikana kama ulaji wa viumbe wa aina moja ndani ya tumbo la uzazi au adelphophagy, neno linalomaanisha “kumla ndugu yako”.

Baada ya kuwala ndugu zao, watoto hao wa papa hupata fursa ya kipekee ya kula mayai yasiyorutubishwa ambayo mama zao huendelea kuyatoa, jambo hili huwafanya wawe na afya njema na nguvu wakati wanapozaliwa.

5. Papa wana marafiki wa karibu

Papa si wawindaji pekee kama wanavyoonyeshwa mara nyingi. Papa wa mwamba wa kijivu hupenda kukaa na kundi moja la marafiki kwa muda wa miaka minne, wakigawanyika katika vikundi vidogo, wakifuata njia zao, na kisha kujipanga upya katika misimu yote.

Papa wachanga wa aina ya limau pia hupenda kuishi katika vikundi na, muhimu zaidi, kujifunza ujuzi mpya kutoka kwa kila mmoja wakati wa mwingiliano huu wa kijamii, kama vile jinsi ya kupata chakula au kuepuka wanyama wanaowinda wanyama wengine. Wanapendelea kukaa na papa wengine wa aina hiyo wa ukubwa wao na wale waliokutana nao hapo awali.

Papa wakubwa wa asilia nyeupe wanaweza hata kuwa na marafiki wa karibu. Kwa kawaida huonwa kuwa wapweke, papa wawili wakubwa weupe, wanaoitwa Simon na Jekyll, walionekana kusafiri pamoja kwa kilomita 6,000 (maili 3,730) bila kutengana.

.

Chanzo cha picha, Hannes Klostermann/ Ocean Image Bank

6. Miili ya papa imefunikwa kwa meno madogo

Ngozi ya papa ni ya ajabu. Katika karne ya 18 Italia, mafundi waliitumia kulainisha kingo laini za violini za Stradivarius. Na huko Uingereza ya Victoria, ikawa nyongeza inayopendwa na watengenezaji wa makabati ambao waliiita “shagreen”.

Badala ya magamba, ngozi ya papa imejazwa na “meno” mengi madogo, yanayoitwa denticles, ambayo yamebanwa kwa mwendo wa mbele wa maji wa kiumbe huyo, na kupunguza mvutano wa angani.

Ukipitisha mkono wako dhidi ya chembechembe na ingekuwa kama kusugua karatasi ya mchanga.

Wakati mwingine papa hugongana na vitu visivyojulikana, wakihisi umbile na uthabiti wao na ukingo mkali wa ngozi yao,aina ya “jaribio la ladha” la vitu ambavyo huenda visiwe chakula.

7. Papa wanaweza kuhisi mapigo ya moyo

Papa wana hisia nane. Mbali na hisia zetu tano za msingi za kuona, kusikia, kunusa na kugusa, pia wana hisia kuu zinazowaruhusu kubaini mabadiliko katika shinikizo au volteji majini, na hata sumaku.

.

Chanzo cha picha, Larsvon Ritter Zahony/Ocean Image Bank

8. Papa ni wakongwe zaidi kuliko miti, pete za Zohali na Nyota ya Kaskazini

Papa ni viumbe wa kale sana. Ushahidi wa awali wa visukuku vya papa wa kale na papa wa leo ni mkusanyiko wa magamba yaliyoanzia miaka milioni 450 iliyopita. Hiyo ni takriban miaka milioni 60 kabla ya miti ya kwanza, milioni 220 kabla ya dinosauri, miaka milioni 350 kabla ya pete za Zohali na miaka milioni 380 kabla ya kuzaliwa kwa Nyota ya Kaskazini.

Meno ya kwanza kama papa yalikuwa miaka milioni 410 iliyopita, na kundi la kwanza lililoonekana kama papa lilibadilika karibu miaka milioni 380 iliyopita. Samaki wengi wa kale huenda hawakuwa papa, lakini walikuwa na uhusiano nao. Kisha, miaka milioni 195 iliyopita, kundi la papa wa kisasa lililojulikana zaidi lilifika, likiwa na taya zao zinazonyumbulika na zinazojitokeza kwa kasi zaidi.

Leo, kuna takriban spishi 500 za papa. Idadi hiyo iko chini sana ya kilele chao karibu miaka milioni 50 iliyopita, ingaw apapa zaidi wanagunduliwa kila uchao.

Kuhusu uhusiano wetu na wanyama hawa wa baharini, papa mkongwe wa kwanza aliishi karibu miaka milioni 440 iliyopita, ingawa alionekana zaidi kama papa kuliko mwanadamu. Kutengana kwetu kunaweza kuwa kuligawanyika milenia zote zilizopita, ila uwepo wetu na wao ni mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *