Kufuatia hujuma za kikatili za jeshi la kigaidi la Marekani dhidi ya madaraja kadhaa katika maeneo ya kusini mwa Iran, operesheni kubwa na endelevu ya makombora na droni za Iran imetekelezwa usiku wa kuamkia leo dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

Ripoti za vyombo vya habari hadi sasa zinaashiria kulengwa kwa kambi za kijeshi za Marekani nchini Bahrain, Kuwait, Qatar, Jordan, na Iraq. Aidha, baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa Daraja la Mfalme Fahd, linalounganisha Bahrain na Saudi Arabia,limelengwa

Saa chache baada ya jeshi la kigaidi la Marekani kushambulia madaraja kadhaa kusini mwa Iran Alhamisi usiku, vyanzo vya habari viliripoti kusikika kwa milipuko mikubwa nchini Kuwait na Bahrain. Afisa mmoja mwandamizi wa Marekani, akizungumza na gazeti la Wall Street Journal, amethibitisha kuwa jeshi la nchi hiyo limelenga madaraja kadhaa nchini Iran kwa lengo la kukata njia za usambazaji wa vifaa kuelekea Bandar Abbas. Daraja la Kahurestan katika kaunti ya Khamir, mkoani Hormozgan, ambalo ni kiungo muhimu kinachounganisha Bandar Abbas na Lar katika mkoa wa Fars, ni miongoni mwa miundombinu liyoharibiwa na mashambulizi ya kigaidi ya Marekani.

Hujuma hizo za kigaidi za Marekani zimesababisha kuuawa na kujeruhiwa kwa raia kadhaa wa Iran. Kufuatia uvamizi huo, mapema Ijumaa, ripoti zilianza kuibuka kuhusu mashambulizi ya Iran dhidi ya ngome za Marekani nchini Kuwait. Jeshi la Kuwait limetangaza kuwa mifumo yake ya ulinzi wa anga imekabiliana na makombora na droni za Iran.

Muda mfupi baadaye, ripoti ziliashiria kuwashwa kwa ving’ora vya tahadhari nchini Bahrain. Vyanzo vya habari vimethibitisha kuwa Kambi ya Tano ya Jeshi la Majini la Marekani nchini Bahrain imelengwa moja kwa moja. Aidha, vyombo vya habari vimeripoti kuwa kambi za Marekani nchini Qatar na Jordan nazo zimewekwa chini ya operesheni hiyo ya kulipiza kisasi.

Hujuma hizo za Marekani dhidi ya Iran ni ukiukaji wa Mkataba wa Islamabad uliosaini baina ya nchi hizo mbili mwezi Juni. Mapatano hayo yalikusudiwa kuweka msingi wa kufungua tena Lango la Hormuz kwa usafirishaji wa kibiashara, kumaliza mapigano, na kuanza mazungumzo kuelekea makubaliano ya mwisho ya amani.

Hata hivyo, Marekani imekiuka makubaliano hayo kwa utaratibu, huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ikitangaza kuwa Washington “imevunja kabisa” sitisho hilo la mapigano.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *