Polisi Tanga yanasa watuhumiwa 200 operesheni maalumuPolisi Tanga yanasa watuhumiwa 200 operesheni maalumu

TANGA: JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limeendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu, baada ya kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 200 katika operesheni maalumu zilizofanyika kuanzia Juni 1 hadi Julai 16, 2026.

Akizungumza leo Julai 17, 2026 Tanga, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, amesema kuwa Katika kipindi hicho cha wiki sita, jeshi hilo limebainisha kuwa hali ya ulinzi na usalama mkoani hapa ni shwari, huku likisisitiza kuwa mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano kati ya polisi na wananchi kupitia falsafa ya polisi jamii.

Katika hatua inayoashiria mwendelezo wa mapambano dhidi ya ukatili na uhalifu uliokithiri Kamanda huyo alisema kuwa jumla ya watuhumiwa 51 walitiwa hatiani na kuhukumiwa vifungo mbalimbali jela baada ya upelelezi wa kesi zao kukamilika.

Aliwataka ambao waliopewa adhabu kali ni Sadiki Waziri , aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya huku Adhabu kama hiyo ya miaka 30 pia imewakuta Julius Mustafa (kwa kosa la kulawiti) na Kilimo Issaya (kwa kosa la kuzini na maharimu).

Wengine waliohukumiwa ni wale waliojihusisha na wizi wa mifugo, ambao wamekabidhiwa vifungo vya miaka mitano kila mmoja, sambamba na wengine waliohukumiwa kwa makosa ya ubakaji, uvunjaji, na uhujumu wa miundombinu.

Aidha Operesheni hizo zimefanikiwa kusambaratisha mitandao ya dawa za kulevya kwa kuwakamata washukiwa 29. Katika msako huo, Polisi walikamata mirungi bunda 750 (kg 45) na bangi iliyokuwa katika misokoto 114, pakiti 126, vifurushi 5, na kete 120.

Aidha, jeshi hilo lilifanikiwa kutaifisha pikipiki 20 zisizo na namba za usajili, vifaa vya miundombinu ya TANESCO na barabara, noti bandia za Kenya, televisheni 10, na simu za mkononi 25, zote zikidhaniwa kuwa mali ya wizi. Vilevile, watu watano walikamatwa wakiwa na nyara za serikali.

Katika jitihada za kupunguza ajali, Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limewakamata madereva 10,028 kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *