Mwanahabari maarufu wa kihafidhina wa Marekani amesema kwamba nchi hiyo inakabiliwa na tishio la mapinduzi ya umma.

“Tuna viongozi ambao hawatuheshimu, wanatudharau, ambao wanatutumia (vibaya), ambao wanatudanganya na hawatujali kabisa,” amesema Tucker Carlson katika mahojiano na Bloomberg.

Ameendelea kusema: “Tunajua vizuri jambo hili, kwa sababu umri wa kuishi unapungua, watu wanakufa wakiwa wadogo, tabaka la kati linatoweka kama ilivyokuwa miaka 11 iliyopita, lakini hakuna anayezungumzia jambo hilo.”

Tucker Carlson amesema: “Mafanikio husababisha uozo, ambao huchea mporomoko na kisha mfumo mpya yaani mapinduzi. Natumai mfumo huo mpya utakuwa wa utulivu ambapo watu watajitambua na kukumbuka kwa nini walifanikiwa hapo awali. Sitaki kutokee mapinduzi, lakini ikiwa mwelekeo huu utaendelea, tutakuwa na mapinduzi.”

Mwanahabari huyo maarufu wa Marekani amesisitiza kuwa: “Mimi napinga utumiaji mabavu wa kisiasa. Ukiwaaminisha watu kwamba kura zao hazina umuhimu na hakuna njia ya kufikisha sauti zao isipokuwa kupitia mabavu na vurugu, basi baada ya muda watu watatumia vurugu. Sitaki suala hilo litukie.”

Carlson alikuwa mshirika wa karibu wa Rais wa Marekani Donald Trump kwa miaka mingi na aliunga mkono Chama cha Republican, lakini baada ya Marekani na Israel kuanza mashambulizi yao makali dhidi ya Iran, alianzisha ukosoaji mkali dhidi ya Ikulu ya Rais wa Marekani, White house na sera za kiongozi wa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *