.

Chanzo cha picha, EPA

Marekani imeanzisha duru nyingine ya mashambulizi ya anga dhidi ya Iran usiku wa kuamkia leo, ikilenga vituo vya ufuatiliaji eneo la pwani ya Iran na mifumo ya ulinzi wa anga.

Kituo kikuu cha kuendesha oparesheni za kijeshi cha Marekani CENTCOM kimesema vikosi vyake vilifanikiwa kushambulia uwezo wa kijeshi wa Iran, huku vyombo vya habari vya serikali ya Iran vikidai kuwa Kisiwa cha Qeshm, kilichopo katika Mlango wa Bahari wa Hormuz, kililengwa.

CENTCOM pia ilisema ililenga Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha Iran (IRGC), ambacho ilikihusisha na shambulio lililosababisha vifo vya wanajeshi wawili wa Marekani nchini Jordan siku ya Ijumaa.

Mwanajeshi mmoja wa Marekani bado hajulikani alipo.

Kujibu mashambulizi hayo, jeshi la Iran limetekeleza mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya kambi mbili za kijeshi za Marekani nchini Kuwait.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *