Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Ndugu Wazo Mwang’onda, leo Julai 21, 2026 amezindua Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Maji katika Kijiji cha Mjiti, Wilaya ya Manyoni, kwa kuweka jiwe la msingi la mradi huo unaolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Mradi huo umegharimu jumla ya shilingi 87,284,483, ambapo Serikali Kuu imechangia shilingi 73,784,483, huku wananchi wakichangia nguvu zenye thamani ya shilingi 13,500,000 katika utekelezaji wake.

Akihitimisha uzinduzi huo, Ndugu Mwang’onda amewahimiza wananchi kuitunza miundombinu ya maji pamoja na kulinda chanzo cha maji ili kiendelee kutoa huduma kwa ufanisi na kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *